Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, July 29, 2014

Mesut Ozil aendelea kula raha za mapumziko marefu ya kiangazi akiwa na kichuna wake Mandy Capristo


Wakati wachezaji wa Arsenal wakijipanga kwa ajili ya kuelekea kwenye Emirates Cup, Mesut Ozil bado anaendelea kula raha za mapunziko akiwa na demu wake.
Ozil mwenye umri wa miaka 25 alionekana akifanya yake akiwa na mpenzi wake Mandy Capristo wakijipunzisha kwa bwawa la kuogelea la hoteli ya kitalii mjini Las Vegas.
Bingwa huyo wa kombe la dunia wa Ujerumani naye kama ilivyo kwa wachezaji wengine wa Ujerumani ambao walipewa mapunziko marefu marefu na vilabu vyao, pia imekuwa hivyo kwa mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid ambaye amepata ruhusa ya bosi wake Arsene Wenger na hatakuwepo kikosini wakati wa kuanza msimu.

Late start: Arsene Wenger says Ozil will miss the beginning of the season to avoid burning out later on
Arsene Wenger amesema Ozil hatakuwepo katika mchezo wa ufunguzi wa msimu.
Relaxed: Mesut Ozil and his girlfriend Mandy Capristo relax after a long season for club and country
Mesut Ozil na mpenzi wake Mandy Capristo wakipumzika baada ya msimu mrefu na klabu yake pamoja na timu ya taifa.
Meneja mfaransa Wenger amekaririwa akisema
'Nimewapa mapumziko wote Ozil, Lukas Podolski na Per Mertesacker mapunziko mazuri kwasababu wachezaji ambao hucheza fainali ya kombe la dunia wanahitaji wanahitaji mapumziko
Arsenal imeelekea Marekani kwa maandalizi ya msimu ambapo ilifungwa na timu ya Thierry Henry ya New York Red Bull bao 1-0.
Arsene Wenger anamatumaini kuwa kikosi chake kitafanya vizuri kiasi katika michuano yao ya mwisho ya maandalizi ya msimu huko Landoni ya Kaskazini ambapo watacheza dhidi ya Benfica mchana na baadaye dhidi ya Monaco siku itakayo fuata.

No comments:

Post a Comment