Matija Nastasic kujiunga kuondoka City |
Manchester
City imepokea maombi ya vilabu vya Inter Milan na Roma kwa ajili ya Matija Nastasic
ambaye wanataka kumuuza kwa lengo la kumsajili Eliaquim Mangala akitokea katika klabu ya Porto.
Hata hivyo inaonekana vilabu hivyo huenda vikapigwa kumbo na Arsenal ambayo inataka kufanya malipo kwa haraka.
Arsene Wenger wanamsaka mlinzi mwingine wa kati endapo nahodha Thomas Vermaelen ataondoka na kujiunga na Manchester United
Mlinzi
huyo wa kimataifa wa Serbia alionekana na thamani kubwa mbele ya
maskauti wa Arsenal alipokuwa akiitumikia Fiorentina, kabla ya City
kumdaka mwaka 2012 na kuendeleza ubora wake kama mlinzi bora Ulaya.
No comments:
Post a Comment