MCHEZAJI wa zamani wa Arsenal na Chelsea Ashley Cole amesema Wachezaji wa England ni waoga kwenda kucheza Klabu za Kigeni.Cole, mwenye Miaka 33, amejiunga na AS Roma ya Italy baada kuondoka Chelsea kufuatia kumalizika kwa Mkataba wake ambao haukuongezwa.
Akiongea na Wanahabari kwa mara ya kwanza kama Mchezaji wa AS Roma, Cole alitamka: “Wachezaji wa Kiingereza pengine wanaogopa kwenda nje ya Nchi, wanajisikia vyema kubaki Nyumbani.”
Kwenye Kikosi cha England kilichokwenda huko Brazil kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia ni Kipa Fraser Forster pekee ndie alikuwa hachezei Klabu ya England lakini nae hakwenda mbali kwani alikuwa Scotland akichezea Celtic.

No comments:
Post a Comment