Manchester
United imetangaza kumsajili mlinda mlango kijana Vanja Milinkovic
katika mpango wake wa kujinasua kutoka katika kipindi cha matokeo mabovu
ndani ya Old Trafford.
Mlinda
mlango huyo mwenye umri wa miaka 17 tayari ameshaiwakilisha Serbia
katika kikosi chake cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 lakini
atasalia katika klabu yake ya sasa ya FK Vojvodina kwa msimu wa 2014-15
akiendeleza kipaji chake.
United
kwasasa ina walinda mlango watatu wazoefu katika kikosi chake ambapo
Anders Lindegaard na Ben Amos wakiwa wanasubiri kwa David de Gea.
Kijana mwenye umri wa miaka 21 Sam Johnstone tayari amekamilisha mpango
wa mkopo katika klabu ya Doncaster.
Red
Devils wanatafuta namna ya kuboresha kikosi chao baada ya kumaliza
katika nafasi ya saba msimu uliomalizika wa Premier League ambao
aliyekuwa meneja wao David Moyes alipoteza kazi kufuatia kushindwa
kutetea taji la ligi hiyo.
Kocha
Mholanzi Louis van Gaal anajipanga kuchukua nafasi ya Moyes na
imefahamika kuwa tayari Van Gaal ameanza kuingiza mipango yake mipya kwa
matayarisho ya msimu ujao ambapo mlinzi wa Borussia Dortmund Mats
Hummels na kiungo wa Roma Kevin Strootmat wakiwa katika orodha ya
wachezaji wake anao wataka.
No comments:
Post a Comment