Akizindua
mashindano hayo, Mkurugenzi mtendaji wa AzamTV, bwana Rhys Torrington
alisema: Lengo kuu la kufanya shindano hili ni kuamsha hisia za
mashabiki wa soka na kuonyesha umuhimu wa kuthamini mashabiki kwa sababu
bila wao mpira wa miguu usingekuwepo leo hii; wakati huo huo ni
kuwaletea watazamaji vipindi vinavyoburudisha na kuelimisha.
Mashindano
haya yametokana na ubunifu wa wafanyakazi wa Azamtv ambapo hiki ni
kipindi kimojawapo kitakachofuatiwa na vingine vingi ambavyo viko ndani
ya maandalizi kupitia kampuni ya Uhai Production ambayo ni kampuni mama
ya AzamTV; aliongeza bwana Wasiwasi Mwabulambo ambaye ni mratibu wa
mashindano hayo.
Wanaoruhusiwa kushiriki mashindano haya ni wanaume wenye umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.
Wakiwa
ndani ya jumba la KWETU HOUSE washiriki wataenguliwa kila siku ya
jumapili mpaka kubakia washiriki watatu ambapo mmoja wao atajinyakulia
kitita cha shilingi milioni kumi (10)
Usaili
wa shindano hili utafanyika siku ya jumamosi tarehe 24/05/2014 uwanja
wa Leaders club, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. Usaili
utakuwa ni bure.
Pia
mashabiki wanaweza kujisajili kwa kutuma video zao fupi kwenda kwenye
whatsApp number 0759 38 65 68 nakuonyesha ushabiki wao wa dhati.
Watakaochaguliwa
watatangazwa tarehe 27/05/2014 ambapo wataingia ndani ya jumba la KWETU
HOUSE tarehe 30/05/2014; na mshindi atapatikana tarehe 27/06/2014.
Shindano hili limedhaminiwa na Azam Energy Drink kwa ushirikiano wa Channel Ten, Magic Fm na Times Fm.
No comments:
Post a Comment