MABINGWA
wa soka wa Tanzania Bara Yanga wameweka historia mpya katika mashindano ya Ligi
ya Mabingwa Afrika baada kuifunga Al Ahly ya Misri kwa bao 1-0 kwenye mchezo
uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kwa
matokeo hayo Yanga itahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote pindi timu hizo
zitakaporudiana katika kipindi cha wiki moja ijayo Cairo, Misri ili isonge
mbele kwa hatua inayofuata ya mashindano hayo.
Yanga
iliingia katika raundi ya pili ya mashindano hayo baada ya kuifunga Comorozine
ya visiwa vya Comoro kwa mabao 7-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa
Taifa Dar es Salaam na kisha kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 kwenye mchezo wa
marudiano.
Shujaa
wa Yanga kwenye mechi ya jana alikuwa nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub’Cannavaro’
aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na kiungo wa kimataifa wa
Rwanda Haruna Niyonzima kwenye dakika ya 81 na kuamsha nderemo na vifijo kwa
mashabiki wa timu waliofurika uwanjani kwenye mechi hiyo.
Ni
miaka 29 imepita tokea timu ya Tanzania kuwafunga mabingwa hao mara nane wa
Afrika kwani mara ya mwisho Simba iliifunga timu hiyo kwa mabao 2-1 kwenye
mchezo mkali uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mwaka 1985 kwa mabao ya
Zamoyoni Mogella na Mtemi Ramadhani.
Cannavaro
ameingia kwenye historia ya nguli hao wa zamani wa kimataifa wa Tanzania kwa
kuweza kufunga bao dhidi ya timu hiyo ambayo wiki iliyopita ilitoka kutwaa taji
la Super Cup kwa kuifunga Csafien ya Tunisia kwa mabao 3-2.
Yanga
ilianza mchezo huo kwa kasi na ilionekana kama wangeweza kupata mabao ya mapema
lakini lakini kipa wa timu hiyo Sherif Ekramy Ahmed aliyokoa mpira wa kichwa
uliopigwa na Emmanuel Okwi kwenye dakika ya 5 na kuwa kona butu.
Al
Ahly walionekana kucheza taratibu na kufanya mashambulizi ya kushtukiza hali
iliyofanya Yanga kutawala mchezo huo kwa kiwango kikubwa na katika dakika ya 20
nusura Hamisi Kiiza aifungie timu yake bao lakini alichelewa mpira wa krosi wa
Simon Msuva toka wingi ya kulia.
Mohamedi
Ismail alikosa nafasi nzuri kwenye dakika ya 28 baada ya kupokea mpira mzuri
uliotokana na shambulizi la kushtukiza kutoka kwa kiungo wa timu hiyo Hossam
Mohamedi akiwa amebanwa na beki Kelvi Yondani alipiga shuti lilitoka pembeni
kidogo ya lango.
Kipindi
cha pili Al Ahly walionekana kuchangamka kidogo hali iliyofanya kutawala mchezo
huo hali iliyomlazimu kocha wa Yanga Hans Pluijm kumtoa Hamisi Kiiza na
kumuingiza Didier Kavumbagu aliyeir ejesha Yanga mchezoni.
Huku
kocha wa Ahly Ahly alimtoa kiungo Moussa Yedan na kumuingiza Mahmoud Ibrahim
hata hivyo ni Yanga walionyesha dhamira ya kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo
huku Al Ahly wakionekana kucheza kwa zaidii kwa kutafuta sare.
Okwi
kwenye dakika ya 70 alipokea pasi nzuri
kutoka kwa Frank Domayo toka katikati ya uwanja aliwazunguka mabeki wa Al Ahly
na kupiga shuti kali lililopanguliwa kipa wa Al Ahly Sherif Ekramy Ahmed na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Kwenye
dakika ya 81 Nadir Haroub’Cannavaro’aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona
uliochongwa na Haruna Niyonzima na kuiandikia Yanga bao hilo muhimu kwenye
mechi hiyo.
Kocha
wa Yanga alimpumzisha winga Mrisho Ngassa na kumuingiza Saidi Bahanunzi huku kocha wa Al Ahly alimpumzisha
Mohamedi Ismail na kumuingiza Ahmedi Shakri mabadiliko ambayo hayakubadili sura
ya mchezo huo.
Yanga
Deogratius Munishi,Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub’Cannavaro’, Kelvin
Yondani, Frank Domayo, Simon Msuva, Haruna Niyonzima , Emmanuel Okwi, Mrisho
Ngassa, Hamisi Kiiza.
Al
Ahly: Sherif Ekramy Ahmed, Saadeldin Saad, Mohamedi Al Ghareeb, Ahmed El
Moneima. Sayed Abdel Wahed, Shihab Eldin Saad, Ramy Abdel Aziz, Moussa Yedan,
Mohamedi Ismail, Amri Gamal Sayed.
No comments:
Post a Comment