Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 1, 2014

MPAMBANO WA DAUDI NA GOLIATH LEO, YANGA INAWEZA KUIFUNGA AL AHLY, UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM? REFA NI HAILEYESUS KUTOKA ETHIOPIA


MABINGWA WA TANZANIA BARA, Yanga, Leo hii watakuwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kuwavaa Mabingwa wa Afrika, Al Ahly, katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONS LEAGUE.

Timu hizi zitarudiana huko Cairo, Misri hapo Machi 9.
Wakati Al Ahly ikiwania kutwaa Ubingwa wao wa 3 mfululizo wa Afrika na ambao utakuwa Ubingwa wao 9, Yanga bado hawajaambua kitu kwenye michuano hii mikubwa Barani Afrika.
Wakati Yanga ipo Nafasi ya Pili kwenye VPL, Ligi Kuu Vodacom, na imepitwa tu na Azam FC kwa vile wamecheza Mechi moja zaidi, Al Ahly, wanaotetea Ubingwa wao wa Misri waliotwaa Mwaka 2011 kwani 2012 Ligi haikuchezwa huko Misri kutokana na vurugu, Msimu huu wapo Nafasi ya 4 baada kufungwa Mechi 3 katika Mechi 9 za Ligi.

Ingawa Al Ahly ni miamba wa kweli wa Afrika, Kihistoria mbinu zao za kucheza Ugenini ni kujihami na kuhakikisha hawafungwi ili ‘waue’ huko Cairo.
Hivyo Mechi hii ya Leo ni wazi mzigo mkubwa utakuwa kwa Washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Supastraika Mrisho Ngassa, ambae alipiga Hetitriki mbili katika Mechi mbili za Raundi iliyopitwa walipoitwanga Komorozine ya Comoro Jumla ya Bao 12-2, pamoja na wenzake Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi.

Ngome ya Al Ahly, chini ya Mkongwe Wael Gomaa, ni imara na wana Wachezaji hatari kina Gedo na Emad Meteb lakini safari hii watamkosa Gwiji Mohammed AbouTrika ambae amestaafu.

VIKOSI VINAWEZA KUWA:
YANGA: Juma Kaseja, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Didier Kavumbagu, Emmanuel Okwi, Hamis Kizza
AL AHLY: Sherif Ekramy, R. Rabia, S. Samir, Wael Goma, S. Moawad, H. Ashour, S. Ahmed, A. Saied, A. Shoukri, R. Sobhi, A. Raouf

REFA:Haileyesus BAZEZEW BAZEZEW BELETE [Ethiopia]
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Kwanza
Jumamosi Machi 1
Dynamos – Zimbabwe v AS Vita Club - Congo, DR
Young Africans – Tanzania v Al Ahly - Egypt
AC Leopards de Dolisie – Congo v Primeiro de Agosto - Angola
Flambeau de l’Est – Burundi v Coton Sport FC - Cameroon
Nkana FC – Zambia v Kampala City Council FC - Uganda
Gor Mahia – Kenya v Espérance Sportive de Tunis - Tunisia
Al Zamalek – Egypt v Kabuscorp - Angola
Kaizer Chiefs - South Africa v Liga Muculmana de Maputo – Mozambique
Stade Malien de Bamako – Mali v  Al-Hilal - Sudan
Jumamosi Machi 2
Enyimba International FC – Nigeria v AS Bamako - Mali
Entente Sportive de Sétif - Algeria v ASFA-Yennenga - Burkina Faso
Berekum Chelsea – Ghana v Al Ahli - Benghazi - Libya
Les Astres de Douala - Cameroon v TP Mazembe - Congo, DR
The Barrack Y.C.II – Liberia v Sewe Sport - Ivory Coast
Horoya Athlétique Club – Guinea v Raja Club Athletic - Morocco

No comments:

Post a Comment