Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 24, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: JUMANNE - OLYMPIACOS vs MAN UNITED, JUMATANO - GALATASARAY vs CHELSEA

Michuano ya UEFA CHAMPIONS LIGI, yanaendelea tena kesho Jumanne na Jumatano wiki hii kwa Mechi nyingine za kwanza 4 za Raundi hiyo ambapo Timu mbili za England, Mabingwa Manchester United na Chelsea, zitakuwa Ugenini kuanza kampeni zao.
Wiki iliyopita, Timu nyingine mbili za England zilianza vibaya kwa zote kufungwa Mechi zao za Nyumbani wakati Man City walipochapwa kwao Etihad 2-0 na Barcelona na kumaliza Mechi wakiwa Mtu 10 baada ya Beki wao, Martin Demichellis, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Hali kama hiyo iliwakuta Arsenal walipopigwa 2-0 Uwanjani kwao Emirates na Bayern Munich na kumaliza Mechi hiyo Mtu 10 baada Kipa wao Wojciech Szczesny kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Wiki hii, Man United watakuwa huko Ugiriki kucheza na Olympiacos na Meneja wao, David Moyes, licha ya kukiri ni Mechi ngumu, amesema wao wamepania ushindi wa huko huko Ugenini.
Wachezaji wa United wakishangilia moja ya bao juzi kwenye mtanange wao na Crystal Palace walipoifunga bao 2-0 ugenini.Solid: David Moyes saw his team pick up a hard earned 2-0 victory at Selhurst ParkKocha David Moyes wa United
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA HIVI:
Olympiakos (4-4-1-1): Roberto, Salino, Manolas, Papadopoulos, Bong, Maniatis, Samaris, Campbell, Fuster, Saviola, Scepovic
Manchester United (4-4-2): De Gea, Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia, Fellaini, Carrick, Januzaj, Rooney, Van Persie
Nao Chelsea watakwenda huko Uturuki kupambana na Klabu Kigogo ya huko, Galatasaray Spor Kulübü, ambayo Straika wake ni Didier Drogba, Gwiji wa zamani wa Chelsea, ambae Mechi yake ya mwisho na Klabu hiyo ya England ni kuifungia Penati ya mwisho katika Mikwaju ya Penati 5 walipoitoa Bayern Munich kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI huko Munich Mwaka 2012 na kutwaa Ubingwa.Lakini Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, amesema urafiki na Drogba utakuwa haupo kwa Dakika 90.Patakuwa hapatoshi...ni Drogba dhidi ya  kocha wake wa zamani

RATIBA:
Jumanne Februari 25
20:00 Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos v Manchester United
Jumatano Februari 26
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC

UEFA CHAMPIONS LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MATOKEO:
Jumanne Februari 18
Manchester City 0 FC Barcelona 2
Bayer 04 Leverkusen 0 Paris Saint-Germain 4
Jumatano Februari 19
AC Milan 0 Atletico de Madrid 1
Arsenal FC 0 Bayern Munich 2

RATIBA:
Jumanne Februari 25
20:00 Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos CFP v Manchester United
Jumatano Februari 26
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC

MARUDIANO
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP

No comments:

Post a Comment