Timu
ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inaendelea kujinoa kwa ajili ya mechi ya marudiano
ya raundi ya kwanza ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia (Shepolopolo)
itakayochezwa Ijumaa (Februari 28 mwaka huu).
Twiga
Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage na Msaidizi wake Nasra Juma inaendelea
vizuri, na kwa mujibu wa programu ya benchi lao la ufundi kesho (Jumatatu),
Jumanne na Jumatano itafanya mazoezi saa 10 jioni.
Mazoezi
hayo yatafanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la
Dar es Salaam. Uwanja huo ndiyo utakaotumika kwa ajili ya mechi hiyo
itakayoanza saa 10 kamili jioni.
Shepolopolo
ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 2-1 wiki iliyopita inatarajiwa kuwasili nchini
Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) kwa ndege ya Fastjet, na siku hiyo hiyo
itafanya mazoezi Azam Complex.
Waamuzi
wa mechi hiyo Ines Niyonsaba, Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana na Suavis
Iratunga, wote kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili nchini Jumatano.
No comments:
Post a Comment