Uchaguzi wa Kamati
ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
utafanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam.
Fomu kwa ajili ya
waombaji uongozi zinaanza kutolewa Februari 24 mwaka huu kwenye
ofisi za Idara ya Habari. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Februari 27 mwaka huu saa 9 alasiri.
Ada kwa wagombea
wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi,
Mhazini na Mhazini Msaidizi ni sh. 50,000 kwa fomu. Nafasi za wajumbe wa Kamati
ya Utendaji fomu zinapatikana kwa sh. 20,000.
Kamati ya Uchaguzi
inawahimiza wanachama wa TASWA kujitokeza kwa wingi kugombea, lakini vilevile
waisome vizuri Katiba ya chama chao.
No comments:
Post a Comment