Mechi
ya pili ya raundi ya kwanza kuwania Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya
Tanzania (Twiga Stars) na Zambia (Shepolopolo) sasa itachezwa Februari 28 mwaka
huu Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Twiga
Stars tayari ipo kambini kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10
kamili jioni. Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage inafanya mazoezi yake
kwenye Uwanja wa Karume ambao ni wa nyasi za bandia kama ulivyo ule wa Azam
Complex.
Shepolopolo
iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14
mwaka huu kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.
Iwapo
Twiga Stars itafanikiwa kuiondoa Shepolopolo itacheza na mshindi wa mechi kati
ya Botswana na Zimbabwe. Zimbabwe ilishinda mechi ya kwanza ugenini.
Wachezaji
wa Twiga Stars waliopo kambini ni Amina
Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe
Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mustafa, Fatuma
Mwisendi, Fatuma Omari, Flora Kayanda, Happiness Mwaipaja, Maimuna Mkane, Mwajuma
Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Pulkeria Charaji, Sherida Boniface, Sophia Mwasikili,
Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.
No comments:
Post a Comment