Lionel
Messi ameshiriki katika michezo minane ya kombe la dunia akiitumikia
timu yake ya taifa ya Argentina. Endapo kama angekuwa anafunga kwa
kiwango chake cha ufungaji kutegemeana na wastani wa ufungaji wake
katika klabu yake ya Barcelona pengine angekuwa amefunga jumla ya magoli
saba katika michezo hiyo nane aliyocheza.
Badala
yake alifunga goli moja tu katika mchezo wa ushindi wa kwa timu yake ya
taifa wa mabao 6-0 dhidi Serbia na Montenegro mjini Gelsenkirchen
mwaka 2006 ndio alifunga goli lake pekee na amekuwa hana aibu licha ya
kukumbana na maneno ya lawama kutoka kwa mshabiki.
Mshindi mara nne wa tuzo ya Ballon d'Or bado anaendelea kukosolewa kwa kutokufunga kwake magoli katika kombe la dunia
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 26 kwasasa anaonekana kuwa mkomavu zaidi na
akiwa akijipabga vizuri kuungana na kikosi cha Argentina kuelekea kwenye
fainali za mwaka huu za kombe la dunia nchini Brazil maarufu kama
'summer's carnival of football' huku wakiingia katika michuano hiyo kama
kikosi kinachopewa nafasi ya pili ya kutwaa taji hilo.
Ananukuliwa akisema
'Slowly
but surely- nitaelekea huko nikiwa na matumaini ya kupanda vema katika
kipindi muafaka cha mwaka' Alikuwa akikaririwa na BBC Football Focus.
'Nadhani huu utakuwa ni mwaka mkubwa si tu kwa upande wangu bali pia kwa klabu yangu ya Barcelona na Argentina.'
Messi
anaamini
kuwa Argentina inaweza kushinda taji la dunia licha ya makabiliano
upinzani kutoka kwa wenyeji Brazil, na anasisitiza michuano hiyo itakuwa
ni ya aina yake kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
'Itakuwa
ni -extra special- kuliko michuano mingine yote ya kombe la dunia
iliyopita, inafanyika Brazil kwenye kila kitu kinachotuwezesha kwa
upande wetu, kwani mashabiki wetu watakuwa pale kwa maelfu na kwa uwepo
wao tunaweza kuvuna kitu -very, very special.'
Hivi sasa: Messi ana magoli 19 katika jumla ya michezo 24 aliyoichezea Barcelona.
Goli moja tu: Goli pekee la Messi katika kombe la dunia alifunga dhidi ya Serbia and Montenegro mwaka 2006
Argentina
haijatinga hatua ya robo fainali katika kombe la dunia tangu mwaka
1990, ambapo walicheza fainali dhidi ya Ujerumani magharibi na kufungwa
kwa bao 1-0 fainali zilipofanyika nchini Italia ambapo kwasasa
wachambuzi wa mambo ya soka wanaamini kuwa tangu wakati huo kikosi cha
nchi hiyo kimeimarika katika siku za hivi karibuni.
Walimaliza katika nafasi ya kwanza katika kundi la CONMEBOL ikipoteza michezo miwili katika jumla ya michezo 16 ya kufuzu.
'Nadhani
kombe hili la dunia linakuja katika kipindi kizuri kwa Argentina.
Tumekua kama timu ndani na nje ya uwanja. Wako wachezaji wengi wanapenda
kucheza kwa ajili ya taifa lao.
'Nadhani tutaelekea Brazil tukiwa vizuri sana na tukiwa na nafasi kubwa ya kushinda taji. Tunajua kombe la dunia ni kitu gani.'
Miaka minne iliyopita: Messi akikabiliana na walinzi wa South Korea katika mchezo wa kombe la dunia 2010 nchini Afrika kusini
Enzi za Maradona: Diego Maradona
akikusanya nusu kijiji cha timu ya taifa ya Belgium mwaka 1982, kama
ilivyo kwa Messi ambaye anaogopwa na duniani kote kwa sasa.
Wachezaji
wakubwa katika soka - Fikiria nyota wa zamani kama Pele, Maradona,
Eusebio -Wote aling'ara na kucheza fainali ya kombe la dunia, hivyo
ndivyo ambavyo Messi anatamani kufanya kwa kufuata nyayo mzaliwa
mwenzake wa Argentina Maradona aliyebeba kombe la dunia mwaka 1986
nchini Mexico.
Yuko
mbali sana katika idadi ya ufungaji katika kombe la dunia wakati Pele
akiwa na rekodi ya mabao 12, Eusebio alifunga magoli tisa.
Kiwango cha mchawi wa soka Pele akiwa na Brazil katika kombe la dunia kilikuwa juu hususani mwaka 1970.
Legendary wa Argentina Maradona
alifunga magoli nane katika kombe la dunia na hivyo kumfanya Messi kuwa
na safari ndefu ya kufikia kiwango cha mzaliwa huyu mwenzake wa
Argentina.
Ubora zaidi unatakiwa: Argentina
ilifika fainali ya kombe la dunia mwaka 1990 ambapo ilifungwa na goli
1-0 na Ujerumani Magharibi nchini Italia, lakini haijafikia nusu fainali
tangu wakati huo na ilishinda kwa mara ya mwisho kombe hilo mwaka 1986
nchini Mexico
'Tulikuwa
na kipindi kizuri cha matokeo ya ushindi katika micheo ya kuwania
kufuzu kwa ushindi wa mchezo wa ugenini nchini Colombia (ushindi wa 2-1
mwezi Novemba 2011) kwangu mimi ulikuwa ni mwanzo mzuri, tumecheza
michezo kadhaa ya kirafiki miongoni mwa hiyo ni dhidi ya vikosi bora
duniani na tulifanya vizuri pia.
'Kwasasa
tunajua ni michuano hiyo ni habari nyingine na lolote linaweza
kutokezea michezo hiyo itakapo anza. Tungependa kuwa na bahati hiyo,
nina matumaini wachezaji wetu watakuwa wakielekea Brazil tukiwa katika
kiwango kizuri kwasababu kwani tutakuwa tukimuhitaji kila mmoja.'
Kiwango cha Messi kipindi hiki kimeshuka, lakini rekodi yake ya magoli 19
katika michezo 24 aliyoichezea klabu yake ya Barcelona kimekuwa kinaimarika.
Majeraha
yamemuweka nje ya uwanja kwa miezi miwili kati ya Novemba na January,
na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anakiri kuwa bado
anajifunza kwa lengo la kujiimarisha zaidi kisoka.
No comments:
Post a Comment