Mechi
ya pili ya raundi ya kwanza kuwania Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya
Tanzania (Twiga Stars) na Zambia (Shepolopolo) itachezwa Machi 2 mwaka huu
Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Twiga
Stars tayari imeingia kambini kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia
saa 10 kamili jioni. Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage inafanya
mazoezi yake kwenye Uwanja wa Karume ambao ni wa nyasi za bandia kama ulivyo
ule wa Azam Complex.
Shepolopolo
iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14
mwaka huu kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.
Iwapo
Twiga Stars itafanikiwa kuiondoa Shepolopolo itacheza na mshindi wa mechi kati
ya Botswana na Zimbabwe. Zimbabwe ilishinda mechi ya kwanza ugenini.
No comments:
Post a Comment