Stand
United ya Shinyanga imekata rufani Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
ikipinga Kanembwa JKT ya Kigoma kuchezesha wachezaji waliosajiliwa katika
dirisha dogo kwenye mechi ya kiporo iliyozikutanisha timu hizo.
Mechi
hiyo namba 22 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilichezwa juzi (Februari 16 mwaka
huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Kanembwa JKT
iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Katika
rufani yake, Stand United inadai kwenye mechi hiyo Kanembwa JKT ilichezesha
wachezaji wanane waliosajiliwa katika dirisha kidogo kinyume na maelekezo
kutoka TFF kwa timu hizo kuwa wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo
hawawezi kucheza mechi hiyo.
Wachezaji
wanaodaiwa kusajiliwa dirisha dogo na kucheza mechi hiyo ni Hamidu Juma,
Ibrahim Shaban Issa, Joseph Mlary, Lucas Charles Karanga, Raji Ismail,
Salvatory Kulia Raphael, Seif Ibrahim Zaid na Yonathan David Sabugowiga.
Dirisha
dogo lilifunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15 mwaka jana, hivyo Stand
United katika rufani yake inaombwa ipewe pointi tatu na mabao matatu kwa
Kanembwa JKT kuchezesha wachezaji wasiostahili.
Awali
mechi hiyo ilichezwa Novemba 2 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga,
na kuvunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya Kanembwa JKT kugomea pigo la
penalti dhidi yao.
No comments:
Post a Comment