Rooney akirejea mazoezini Jumatano baada ya siku tano za maaandalizi mjini Dubai |
Wayne
Rooney amekubaliana kimsingi pamoja na mambo mengine mshahara wa pauni
£300,000 kwa wiki lakini mpango huo ukisubiri kusaniwa mpaka hapo
mustakabali wa haki za mauzo picha yake utakapo fikiwa.
Imefahamika
kuwa mshambuliaji huyo wa United akiwa sambamba na mwakilishi wake kwa
pamoja wamefurahishwa malipo mengine manono ikiwemo mshahara na
marupurupu mengine ya bonasi.
Wayne Rooney kupokea £300,000 kwa wiki United
Hivyo,
Rooney hatasaini mpango huo wa nyongeza ya mkataba wake mpya mpaka hapo
makubaliano yatakapo fikiwa juu ya haki za mauzo ya picha yatakapo
fikiwa.
Mtendaji
mkuu wa United Ed Woodward ana imani kuwa suala hilo litafikiwa muafaka
mpaka kufikia Alhamisi au Ijumaa na kuna nafasi nyingine ya kumsainisha
mshambuliaji huyo mkataba wa miaka mitano na nusu mpaka kufikia Ijumaa.
Endapo
halifanyika katika kipindi hicho, italazimika kusubiri mpaka United
itakapo rejea kutoka katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya nchini Ugiriki
wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment