MENEJA
wa zamani wa klabu ya Swansea City, Michael Laudrup amedai kuwa
alitimuliwa kwa barua pepe saa chache baada ya kuambiwa kibarua chake
kiko salama na kushikana mikono na mwenyekiti wa klabu hiyo Huw Jenkins.
Laudrup mwenye umri wa miaka 49 aliiongoza klabu hiyo kunyakuwa Kombe
la Ligi msimu uliopita likiwa ni taji la kwanza kubwa kwa timu hiyo
katika hitoria yao ya miaka 102. Hata
hivyo alitimuliwa mwezi huu baada ya matokeo mabovu ya timu hiyo na
kutokuelewana kwa benchi lake la ufundi. Kocha huyo amesema jambo hilo
la kutimuliwa kwa kupewa barua pepe lilimchanganya sana kwani lilitokea
muda mchache baada ya kuhakikishiwa kibarua chake huku akipeana mkono na
Jenkins. Laudrup ambaye pia amewahi kuinoa Real Mallorca ameendelea
kudai kuwa alifanya mazungumzo na Jenkins na kumtaka kufukuza benchi
lake la ufundi lakini alimkatalia hatua ambayo ilipelekea kutimuliwa
siku moja baadae.
Wachezaji wa Swansea wakiwa wamebeba kombe la Capital One Cup msimu uliopita mwezi Februarikwa sasa ni Garry Monk
Wachezaji wa Swansea wakiwa wamebeba kombe la Capital One Cup msimu uliopita mwezi Februarikwa sasa ni Garry Monk
No comments:
Post a Comment