Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 25, 2014

KOMBE LA MATAIFA YA ULAYA UEFA 2016

Kwa upande wa kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kitaanza kusaka nafasi ya kushiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2016 dhidi ya Scotland. Upangaji wa makundi ulifanywa jana Jumapili mjini Nice , unaonesha kuwa kikosi hicho cha kocha Joachim Loew kitakumbana na Poland Oktoba 14 na kisha kitakutana na Ireland nyumbani baadaye katika kundi D.
Timu nyingine katika kundi hilo ni kikosi kipya katika soka la Ulaya cha jimbo la Gibralter. 
Gibralter ilikubaliwa kuwa mwanachama mpya wa UEFA mwaka jana na ilibidi kubadilishwa kundi baada ya kupangwa katika kundi moja la C na Uhispania, nchi ambayo inadai kuwa jimbo hilo ni lake. Hatua hiyo inaziweka Uhispania na Uingereza katika mvutano mkubwa, ambapo nayo Uingereza inadai kuwa Gibralter ni jimbo lake.
Mchezo wa mwisho wa kufuzu kwa ajili ya fainali hizo zitakazofanyika nchini Ufaransa kuanzia Juni 10 hadi Julai 10 mwaka 2016 utakuwa Oktoba 8 , 2015 dhidi ya Irland na Oktober 11, 2015 dhidi ya Georgia. 

 Group A
Netherlands, Czech Republic, Turkey, Latvia, Iceland, Kazakhstan

Group B
Bosnia and Herzegovina, Belgium, Israel, Wales, Cyprus, Andorra

Group C
Spain, Ukraine, Slovakia, Belarus, Former Yugoslav Republic of Macedonia, Luxembourg

Group D
Germany, Republic of Ireland, Poland, Scotland, Georgia, Gibraltar

Group E
England, Switzerland, Slovenia, Estonia, Lithuania, San Marino

Group F
Greece, Hungary, Romania, Finland, Northern Ireland, Faroe Islands

Group G
Russia, Sweden, Austria, Montenegro, Moldova, Liechtenstein

Group H
Italy, Croatia, Norway, Bulgaria, Azerbaijan, Malta

Group I
Portugal, Denmark, Serbia, Armenia, Albania

Bye to finals (hosts): France
Kocha wa Ujerumani Joachim Loew
Kocha Joachim Loew alikuwa na haya ya kusema.
"Nafikiri , tukiangalia kwa upande wa kimichezo, ni hali ya kuvutia, lakini pia inagusa hali halisi, pamoja na shauku. Kwa Ireland na Scotland, hapa tunafahamu la kufanya, kwa kuwa tunajua jinsi timu hizi zinavyocheza.
  Kwa hiyo nafikiri ni kundi la kuvutia kwetu. Tumekuwa kila mara na kiwango, cha kuweza kushinda katika makundi na pia kufuzu kucheza katika fainali."
Kwa upande wa Gibralter nchi ambayo ina wakaazi 30,000 ni kibarua kigumu sana kuweza kufuzu kwa ajili ya fainali hizi zitakazokuwa na washiriki 24 mara hii nchini Ufaransa, lakini Gibralter ina shauku kushiriki katika zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment