MENEJA
wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa hatua za
kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya Olivier Giroud baada ya kuomba radhi
kwa kumuingiza mwanamke katika chumba cha hoteli ilipofikia timu hiyo. Mara
kwa mara Giroud amekuwa akikataa kumchukua Celia Kay katika Hotel ya
Four Seasons iliyopo Canary Wharf usiku mmoja kabla ya mchezo wao dhidi
ya Crystal Palace ambao walishinda mabao 2-0 Februari 2 mwaka huu. Mapema
nyota huyo aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wake wa kijamii wa
twitter akimuomba radhi mke wake Jennifer na bosi wake Wenger baada ya
picha ya mrembo huyo kutokea katika gazeti. Akihojiwa Wenger amesema
suala hilo ni la ndani hivyo hataki kuliweka hadharani kwasababu
anaheshimu mambo yake binafsi. Picha iliyopigwa na mrembo huyo katika
chumba alichofikia Giroud akiwa na nguo ya ndani pekee ilichapishwa
katika gazeti la The Sun Jumapili iliyopita. Mrembo huyo mwanamitindo wa
majarida ya kimataifa kama Maxim na FHM alipigwa picha akiingia
hotelini hapo akiingia na akitoka katika mida mibovu ya usiku wa manane
huku mwenyewe akimshangaa Giroud kukana kujirusha naye usiku huo.
The model was pictured arriving and leaving the Arsenal team hotel just hours before their match against Crystal Palace
Revelations: Kay revealed her meeting with Giroud last week but the striker denied any wrongdoing
The model was pictured arriving and leaving the Arsenal team hotel just hours before their match against Crystal Palace
No comments:
Post a Comment