Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 18, 2014

KOMBE LA DUNIA-BRAZIL, DAKTARI MKUU FIFA AONYA: “TUTAKUJA WAKATI WOWOTE, MAHALI POPOTE”

WACHEZAJI wote watakaoshiriki Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka huu huko Brazil watapimwa ikiwa wanatumia Madawa ambayo ni marufuku kabla ya Fainali hizo kuanza hapo Juni 12 kwa kumujibu wa Daktari Mkuu wa FIFA, Jiri Dvorak.
FIFA wanataka Timu zote 32 zitakazoshiriki Fainali hizo za Brazil kutuma Ratiba yao ya wapi Timu zao zitakuwepo kabla Machi 1 kwao ili waweze kujua wakati gani Wachezaji hao watapimwa.

Hata hivyo, Jiri Dvorak ameeleza Wachezaji hao na Timu zao hawatajua ni wakati gani Wapimaji watatua Kambini mwao na watahakikisha kuwa hakuna Timu itakayokwepa kupimwa kabla ya Mechi ya Ufunguzi kati ya Wenyeji Brazil na Croatia hapo Juni 12.

Dvorak amesema: “Nina furaha kuwa Watu wana wasiwasi udhibiti wa Madawa Marufuku utaanza lini kwa sababu hatutangaza. Tutakuja wakati wowote, mahali popote!”

Aliongeza: “Kuanzia Machi 1, tutaomba tujue Ratiba ya Timu zitakuwa wapi. Na sisi Makao Makuu tutaamua wakati gani tutazifuata. Kwa kuweka wazi, tutawapima Wachezaji wote si chini ya mara moja kabla ya Mechi ya Kwanza!”

No comments:

Post a Comment