Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 18, 2014

ELIZABETH MICHAEL "LULU" AFIKA MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM


Elizabeth Michael ‘Lulu’
  STAA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametinga ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiambatana na msanii maarufu wa filamu Bongo, Mahsein Awadh 'Dk. Cheni' 
Siku ya leo Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam ilikuwa ikimsomea shitaka mwigizaji maarufu wa Bongo Movie, Elizabeth Michael LULU la kuua bila kukusudia msanii wa maigizo Steven Kanumba mnamo April 07 mwaka 2012 eneo la Vatican Sinza jijini Dar es salaam.
Lulu akiwa na Dr.Cheni pamoja na mama yake mahamani
Hata ivyo wakili anayemtetea LULU, Peter Kibatala alisema kwamba wameridhishwa na sehemu kubwa ya maelezo ya awali ya mteja wao ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka itakapopangwa tena huku kila upande ukitarajia kuleta mashahidi watatu.

No comments:

Post a Comment