MWENYEKITI wa Organizesheni ya Ngumi cha Kulipwa
(TPBO), Yassin Abdalla (Ustaadh) ateuliwa kuwa Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati
(ECAPBA)
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati
(ECAPBA) katika kikao chake kilichokaa
Januari 4, mwaka huu, jijini
Kigali, Rwanda, lilifanya mabadiliko ya kujaza nafasi za uongozi.
Akizungumza jijini, Afisa Habari wa ECAPBA, Boniface Wambura alisema kuwa Yassin Abdalla (Ustaadh) wa Tanzania ameteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa ECAPBA.
Akizungumza jijini, Afisa Habari wa ECAPBA, Boniface Wambura alisema kuwa Yassin Abdalla (Ustaadh) wa Tanzania ameteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa ECAPBA.
Abdalla ambaye ni Rais wa TPBO amejaza nafasi
ya Celestino Mindra wa Uganda aliyekuwa Rais wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya
Madola na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa ya Uganda (UPBC), Simon Kategole wa Uganda, ameteuliwa kuwa
Katibu Mkuu wa ECAPBA kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Shaban Ogolla wa Kenya
ambaye yuko masomoni nchini Marekani. Daudi Chikwanje wa Malawi anachukua
nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa ECAPBA.
Aidha,
Nelson Sapi wa Zambia ameteuliwa kuwaNaibu Mweka Hazina wa ECAPBA akimsaidia
Nemes Kavishe wa Tanzania na Boniface Wambura wa Tanzania anabaki kuwa Afisa
Habari wa ECAPBA wakati wajumbe wanne wameongezwa kwenye Kamati ya Utendaji
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Malawi na Ethiopia pamoja na Roman
Chuwa wa jiji la Arusha.
Aidha,
ECAPBF inamshukuru Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo kwa kukubali
kuwa mlezi wake na kuipatia ofisi katika Manispaa ya jiji la Arusha ikikumbukwa
kwamba ndicho chombo cha kuwaunganisha vijana cha Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC). Katika malengo yake, ECAPBA itafanya kazi kwa karibu sana na Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki (EAC) ili iweze kuwa chachu ya utekelezaji wa maamuzi ya
Jumuiya katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati.
Pia Wambura alisema ECAPBA itafanyia utekelezaji maamuzi yote yanayohusu maendeleo ya vijana pamoja na ushirikiano wa utamaduni na michezo wa EAC kama yaliyopendekezwa na jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kutengeneza ajira kwa vijana wa Afrika Mashariki na Kati.

No comments:
Post a Comment