Kocha
mkuu wa wekundu wa Msimbazi Simba Mcroatia Zdravko Logarusic ameuomba
uongozi wa wekundu hao kumpatia michezo miwili zaidi ya maandalizi kabla
ya kuingia katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara
maarufu kama ligi kuu ya Vodacom.
Logarusic
ameomba michezo hiyo ikiwa ni siku moja tu mara baada ya kurejea kutoka
visiwani Zanzibar ambako Simba walikuwa wakishiriki michuano ya
kuadhimisha miaka hamsini ya mapinduzi ya Zanzibar ambako Simba
ilifanikiwa kufika fainali na kufungwa na KCC ya Uganda kwa bao 1-0.
Akiongea mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, kocha
msaidizi wa wekundu hao Selemani Matola amesema bosi wake ameuomba
uongozi kumtafutia michezo miwili ya maandalizi zaidi, huku mchezo mmoja
ukiwa na timu ya nchini Tanzania na mchezo mwingine dhidi ya timu
kutoka nje ya nchi.
Matola
amesema kimsingi wamekubali matokeo ya mchezo wa fainali na kwamba
wanatengeneza kikosi kwa ajili ya ligi hivyo basi michezo hiyo
itawasaidia kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye michuano ya kombe
la mapinduzi.
No comments:
Post a Comment