Anderson anaondoka Manchester United kwenda Fiorentina kucheza ligi ya Serie A.
Kiungo aliyekuwa hana nafasi na aliyekuwa hatakiwi kuendelea kuwepo Manchester United Anderson Luís de Abreu Oliveira ameelekea nchini Italia kujiunga na Fiorentina akitangulia kufanyiwa vipimo vya afya yake ikiwa ni mpango wa uhamisho wake wa mkopo wa kujiunga na kikosi hicho kinacho shiriki ligi kuu ya nchini Serie A.
Kiungo huyo raia wa Brazil amewaeleza marafiki zake kuwa alikuwa akisaka uhamisho wa kudumu kujihakikishia muda zaidi wa kucheza soka lakini United ndio waliomkwamisha kwa kumuondoa klabu hapo kwa mkopo.
Anderson alionekana Frankfurt mapema asubuhi ya leo akiwa akiwa katika zoezi la kuunganisha ndege akitokea Manchester mpango wake wa uhamisho ukitarajiwa kukamilishwa hapo kesho Ijumaa.
Alijiunga na Klabu ya Manchester United
mwaka 2007 akitokea Porto kwa kitita cha £20million, Amecheza Mechi 179
na mpaka sasa amefunga bao tisa tu.
Kwa upande wao Fiorentina wana majeruhi ya akina Giuseppe Rossi na Mario Gomez hivyo wamekuwa wakiwasiliana na vilabu vya Premier League kusaka washambuliaji huku kutoka AS Roma wakimkodolea macho Marco Borriello na kutoka Juventus wachezaji wawili Mirko Vucinic Fabio Quagliarella.

No comments:
Post a Comment