TIMU ya Simba leo imeifunga Yanga
mabao 3-1 kwenye mchezo wa nani mtani jembe na kuondoka na kitita cha milioni
100, medali za dhahabu na kombe.
Simba ambayo haikupewa nafasi kubwa
ya kushinda mchezo kabla ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Amis Tambwe
aliyefunga mawili huku Juma Awadh akipigilia msumari wa mwisho.
Katika
mchezo huo Simba ilianza kuhesabu bao lake la kwanza katika dakika ya 13
lilofungwa na Tambwe baada ya kazi nzuri ya Ndemla.
Wakati Yanga
ikijaribu kutaka kusawazisha bao hilo, Simba ilifunga bao la pili kwa mkwaju wa
penalti dakika ya 42 iliyofungwa na Tambwe baada ya David Luhende kumuangusha
Ramadhani Singano eneo la hatari.
Katika
kipindi cha pili, uzembe wa golikipa mpya wa Yanga, Juma ulimuwezesha Awadh Juma
kuifungua kirahisi Simba bao la tatu.
Yanga
ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji aliyesajiliwa hivi
karibuni, Emmanuel Okwi aliyefunga kwa kichwa dakika ya 89 akiunganisha krosi
ya Haruna Niyonzima.
Timu zote
zilifanya mabadiliko ya wachezaji katika kipindi cha pili, ambapo Simba
iliwatoa, Henry Joseph, Ndemla, Chanongo, Awadh na Ramadhani Redondo, huku
nafasi zao zikichukuliwa na Singano, Seleman Uhuru, Zahoro Pazi na Humud.
Huku Yanga
ikiwatoa, Athuman Idd ‘Chuji’, Hamisi Kiiza, Didier Kavumbagu, Haroub Cannavaro
na Mrisho Ngassa, huku nafasi zao zikichukuliwa na Emmanuel Okwi, Simon Mvusa,
Dilunga,Juma Abdul na Jerryson Tegete.
Katika
mchezo huo, Yanga ilimpoteza Kelvin Yondani aliyooneshwa kadi nyekundu kwa
kumchezea vibaya, Singano.
No comments:
Post a Comment