Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, December 22, 2013

SWANSEA CITY 1 vs EVERTON 2, ROSS BARKLEY AIPANDISHA EVERTON NAFASI YA NNE

Ross Barkley, amefunga Bao katika Dakika ya 84 kwa Frikiki murua nakuipa ushindi Everton walipoichapa Swansea City, waliokuwa kwao Liberty Stadium, Bao 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Bao la kwanza la Mechi hii lilifungwa kwa kiki kali ya Fulbeki wa Everton, Coleman, katika Dakika ya 66 lakini lilidumu kwa Dakika 4 tu kwani Fulbeki wa Swansea, Tiendalli, alipanda juu na jaribio lake lililokuwa linaenda nje kumbabatiza Oviedo na kutinga na kuifanya Gemu iwe 1-1.

Ndipo ikaja Frikiki ya Ross Barkley iliyowapa ushindi Everton na kuwafanya wawe hawajapoteza Mechi yeyote katika Mechi 10 na kupanda hadi Nafasi ya 4 kwenye Msimamo wa Ligi.
Steven Pienaar na  Ben Davies wakichuana vilivyo leo kwenye ligi kuu EnglandMajanga: Jose Canas na Gareth BarryWilfried Bony na Barkley wakionesha ubabe nani akatize nani apoteze mpiraWakipoteza nafasi ya kufunga bao...na hapa mchezaji anajiuliza zaidi kupoteza nafasi hiyo iliyokuwa waziBaadae Everton wakazinduka na mchezaji Seamus Coleman akaipatia baoRaha ya ushindi kupongezwa!!! baada ya kupata bao hapaSwansea wakisawazisha bao na hapa anashangilia bao2-1 mpaka ndani ya nyavu..

No comments:

Post a Comment