

Chester ndie alieipa Hull Bao la kuongoza na ndani ya Dakika 13 waliongoza Bao 2-0 baada ya Shuti hafifu la David Meyler kumbabatiza Jonny Evans na kumhadaa Kipa De Gea.

Lakini Man United walizinduka na Chris Smalling kuunganisha kwa kichwa frikiki nzuri ya Wayne Rooney na kufunga Goli la Kwanza na Dakika 7 baadae Wayne Rooney aliisawazishia Man United kwa Bao tamu baada kusogezewa na Danny Welbeck.

Hilo ni Bao la 150 kwa Rooney kwenye Mechi za Ligi akiwa na Man United na kumfanya awe Mechezaji wa Pili kufikisha idadi hiyo akichezea Klabu moja tu na mwingine ni Thiierry Henry aliekuwa Arsenal na kufunga Bao 175.

Hadi Haftaimu Bao zilikuwa 2-2 na ndipo Kipindi cha Pili Chester alipojifunga kwa kichwa baada kuicheza krosi ya Ashley Young iliyokuwa ikielekea kwa Rooney.
Valencia alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwenye Dakika ya 90 baada kupewa Kadi ya Njano ya Pili kwa kupoteza muda kwa makusudi.




















RATIBA/MATOKEO:
Alhamisi Desemba 26
Hull City 2 Man United 3 FT
Aston Villa 0 v Crystal Palace 1
Cardiff 0 v Southampton 3
Chelsea 1 v Swansea 0
Everton 0 v Sunderland 1
Newcastle 5 v Stoke 1
Norwich 1 v Fulham 2
Tottenham 1 v West Brom 1
West Ham 1 v Arsenal 3
20:30 Man City v Liverpool
No comments:
Post a Comment