Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 9, 2013

NIYONZIMA AWABWAGA AKINA KIEMBA KWENYE TUZO YA MWANASOKA BORA


Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga kushoto akimkabidhi tuzo ya Ufungaji Bora mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast katika tuzo za gazeti la Mwanaspoti usiku wa jana ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa TEKNOHAMA, Januari Makamba kushoto akimkabidhi tuzo ya Mwanasoka Bora, kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima kulia. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya MCL, Zuhura Muro


Rais wa heshima wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Said El Maamry akimkabidhi tuzo ya Mchezaji bora wa Tanzania anayecheza nje, mwakilishi wa mshindi wa tuzo hiyo, Mbwana Samatta wa TP Mazembe ya DRC.


Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Geoffrey Nyange 'Kaburu' akimkadhi tuzo Refa Bora, Oden Mbaga


Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Zamoyoni Mogella akimkabidhi tuzo ya bao bora, mwakilishi wa mshindi wa tuzo hiyo, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC


Juma Kaseja, akipokea Tuzo ya 11 Bora kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya MCL, Zuhura Muro kushoto


Amri Kiemba wa Simba SC akipokea tuzo ya 11 Bora


Winga wa Azam FC, Joseph Kimwaga akipokea tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi kutoka kwa Mohammed Rweyemamu, Mjumbe wa Bodi ya MCL 


Mwanahaisi Omar akipokea tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike kutoka kwa Makamu Rais wa Shirikisho la Soka la Wanawake (TWFA), Rose Kisiwa kushoto


Makamba akimkabidhi tuzo ya heshima, Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Nicholaus Akwitende kulia 


Nahodha mwingine wa zamani wa Taifa Stars, John Lyimo akipokea tuzo ya heshima kulia


Nahodha mwingine wa zamani wa Taifa Stars, Mbwana Abushiri akipokea tuzo yake


Nahodha mwingine wa zamani Taifa Stars, Omar Zimbwe akipokea tuzo yake ya heshima


Mchezaji wa zamani wa Taifa Stars, Said George aimpokelea tuzo Jellah Mtagwa


Mtangazaji maarufu wa mpira wa zamani wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), sasa TBC, Mzee Mshindo Mkeyenge (katikati) akipokea tuzo yake ya heshima


Meneja Uhusiano wa Vodacom, Salum Mwalimu akimkabidhi Tenga tuzo ya Utawala Bora


Wachezaji na wawakilishi wa wachezaji walioteuliwa katika 11 Bora ya gazeti la Mwanaspoti wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushinda tuzo zao


Mzee King Kiki alitumbuiza 


Rapa Joh Makini akitumbuiaza


Rapa Joh Makini akiwataka waalikwa wainue mikono juu


Na kweli watu wazima waliiua mikono kucheza Hip hop


Rapa Juma Nature akitumbuiza


Ofisa wa Azam FC, Patrick Kahemele akipokea tuzo ya 11 Bora kwa niaba ya Kipre Tchetche


Juma Kaseja na Amri Kiemba baada ya kupokea tuzo zao


Msanii akionyesha utundu na kipaji cha kunyumbulika


Hivi ni vipaji adimu


TBC1 walikuwa live jana


Amerudi Yanga huyu; Kipa wa Coastal Union, Shaaban Kado kushoto akifurahia jambo na Juma Kaseja


Kutoka kulia kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi, kiungo wa Coastal Union, Uhuru Suleiman ma mwigizaji Elizabeth Michael 'Lulu'


Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Ally Mayay kulia akiwa na Kaburu


Ni haki yake kuchoka; Boniface Wambura kulia, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF anafanya kazi sana na haikuwa ajabu aliishia kusinzia kwa uchovu jana wakati wa shetehe za tuzo, kushoto ni Mogella.

Kwa hisani ya Bin Zubeiry

No comments:

Post a Comment