Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 10, 2015

ARSENAL ILIPOIFUNGA OLYMPIACOS 3-0 UEFA CHAMPIONS LEAGUE

SAFU ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, imekamilika Jana na Timu za England, Arsenal na Chelsea, zilishinda hapo Jana na kutinga Mtoano.
Timu hizo zinaungana na Chelsea iliyofuzu mapema ikiwa na Mechi 2 mkononi.

Juzi Man United ilitolewa UCL na kutupwa UEFA EUROPA LIGI baada ya kumaliza Nafasi ya 3 kwenye Kundi B.
Man United sasa itacheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya Kombe hilo.
Droo za kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya UCL na ile ya EUROPA LIGI itafanyika Desemba 14.
Giroud akishangilia mbele ya Meneja Wenger
Olivier Giroud alifungia Arsenal mabao matatu kwa mara yake ya kwanza na kuhakikisha Gunners wanaendeleza rekodi yao nzuri Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kufika hatua ya 16 bora kwa kulaza Olympiakos.
Arsenal walihitaji kushinda kwa mabao mawili wazi lakini walipata mabao hata zaidi na kumaliza wa pili Kundi F.
Giroud alianza kwa kufunga kwa kichwa kipindi cha kwanza, kisha akafunga la pili kipindi cha pili kwa usaidizi kutoka kwa Joel Campbell.
Mfaransa huyo alihakikisha Arsenal wanafuzu kwa kufunga la tatu kupitia penalti.
Man Utd kucheza Europa League
Arsenal hawajawahi kukosa kufika hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tangu kuanza kwa mfumo wa sasa 2003-4, na walionyesha uzofu wa kusakata gozi katika jukwaa kuu Ulaya kwa kung’aa Athens.

Takwimu muhimu:
Olivier Giroud ndiye mchezaji wa nne kufungia Arsenal hat-trick kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (baada ya Thierry Henry, Nicklas Bendtner na Danny Welbeck).
Vijana wa Arsene Wenger wameshinda mechi yao ya kwanza Ugiriki tangu Desemba 1998 (3-1 dhidi ya Panathinaikos).
Giroud ndiye mchezaji was aba wa Arsenal kufikisha magoli kumi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (wengine wakiwa Henry, van Persie, Ljungberg, Fabregas, Walcott na Pires the others).
Matokeo ya Jumatano yalifikisha kikomo msururu wa kutoshindwa wa Olympiakos wa mechi sita katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya timu za Uingereza(Kushinda 5, Sare 1)
Arsenal walikuwa wameshindwa mechi tatu zao za awali ugenini dhidi ya Olympiakos zote katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, zote katika mechi ya sita hatua ya makundi.Bao hilo lilifungwa kwa kupitia mkwaju wa penatiKipa Roberto hakuona ndaniGiroud akishangilia bao lakeGiroud pia ndie aliyefunga bao la pili na kufanya 2-0Pongezi zikiambatana na mshangao!Meneja Arsene WengerFlamini na Kassami wakigombea mpira wa kichwaKikosi cha ArsenalArsene Wenger na Msaidizi wake Kabla ya Mechi