Thursday, November 7, 2013
MBEYA CITY NA AZAM FC KUAMUA NANI WA KUKAA KILELENI HADI MZUNGUKO WA PILI NA YANGA KULINDA HESHIMA KWA JKT OLJORO
Mbeya city leo itakuwa wageni wa Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara utakaochezwa kwenye uwanja wa Chamazi uliopo Mbande, mtanange utakaoonyeshwa Live na kituo cha Azam media kupitia TBC 1 wakati Yanga wao watakuwa Taifa wakicheza na timu dhoofu ya JKT Oljoro toka Arusha.
Mchezo wa Azam na Mbeya City ndio mchezo ambao umevuta hisia za mashabiki kutokana na timu hizo kutopoteza mchezo hata mmoja huku zikiwa na pointi 26 kila moja zikitofautiana kwa mabao ya kufunha na kufungwa.
Hivyo matokeo katika mchezo huo ndio yataamua nani atashika usukani wa Ligi Kuu kwani atakayeshinda atafikisha pointi 29 ambazo Yanga haitaweza kuifikia hata ikiifunga JKT Oljoro.
Pia Mbeya City na Azam FC zikitoka sare na Yanga kushinda mchezo wake basi hakuna ubishi vijana hao wa jangwani watakwenda mapumziko wakiwa vinara kwa kufikisha pointi 28 hivyo tusubiri matokeo ya dakika 90.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment