Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia Jeshi la Polisi kuanzia sasa
halitashikilia silaha za washabiki, na badala yake litawazuia kabisa kuingia
viwanjani wakati wa mechi.
Jeshi la Polisi
limekuwa likihifadhi silaha za washabiki wanaokwenda viwanjani, na baadaye
kuwarejeshea baada ya mechi kumalizika kwa vile Kanuni za Usalama Viwanjani za
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) zinakataza silaha viwanjani.
Wikiendi iliyopita
katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jeshi la Polisi lilikamata bastola 17
katika upekuzi wa washabiki waliokwenda kushuhudia mechi kati ya Yanga na Ruvu
Shooting na ile kati ya JKT Ruvu na Simba. Wote waliokutwa na silaha hizo
walikuwa na leseni za kuzimiliki.
Hivyo, kwa
washabiki wanaomiliki silaha hatawaruhusiwa kabisa kuingia viwanjani, na badala
yake tunawashauri kuzihifadhi huko wanakotoka kabla ya kufika viwanjani.
Pia tunatoa mwito
kwa shabiki ambaye atamuona mwenzake akiwa na silaha uwanja kutoa taarifa kwa
mamlaka husika likiwemo Jeshi la Polisi ili aweze kuchukuliwa hatua.
No comments:
Post a Comment