SIMBA KUIVAA
RUVU SHOOTING VPL
Michuano ya Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya saba
kesho (Oktoba 5 mwaka huu) kwa mechi nne ambapo Ruvu Shooting itakuwa
mwenyeji wa vinara Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio katika
mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mohamed Theofil kutoka Morogoro kuanzia
saa 10 kamili jioni vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Tiketi zitauzwa uwanjani kuanzia saa 4 asubuhi.
Mechi nyingine za
kesho ni JKT Ruvu itakayoumana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam huku
Coastal Union ikiwa mwenyeji wa Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha ndiyo utakaotoa fursa kwa
timu za Oljoro JKT na Mbeya
City kuoneshana ujuzi
katika kusaka pointi tatu.
Ligi hiyo
itaendelea Jumapili (Oktoba 6 mwaka huu) kwa mechi kati ya Yanga na Mtibwa
Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam wakati Mgambo Shooting itaialika Tanzania
Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
FDL KUTIMUA
VUMBI VIWANJA KUMI
Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) kuwania tiketi za kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao
(2014/2015) inaendelea wikiendi hii (Jumamosi na Jumapili) kwa kuzikutanisha
timu 20 zitakazopambana katika viwanja kumi tofauti.
Jumamosi kutakuwa
na mechi kati ya Green Warriors na Friends Rangers (Uwanja wa Mabatini,
Mlandizi), Kimondo na Burkina
Faso (Uwanja wa CCM Vwawa, Mbozi), Mlale JKT
na Mkamba Rangers (Uwanja wa Majimaji, Songea) na Kurugenzi dhidi ya Polisi
Morogoro (Uwanja wa Wambi, Mafinga).
Polisi Dodoma na
Stand United (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Toto Africans na JKT Kanembwa (Uwanja
wa CCM Kirumba, Mwanza), Mwadui na Polisi Mara (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga)
na Polisi Tabora na Pamba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
Keshokutwa
(Jumapili) kutakuwa na mechi kati ya African Lyon na Transit Camp (Uwanja wa
Mabatini, Mlandizi) na Villa Squad dhidi ya Polisi Dar es Salaam (Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam).
No comments:
Post a Comment