London,
England
Arsene Wenger huenda
akazidi kuwachefua mashabiki wa timu hiyo, baada ya kusisitiza kuwa hawana haja
ya kupaniki kutokana na Arsenal kutokusajili, kwani Nicklas Bendtner atarejea
Emirates kuziba pengo katika safu ya ushambuliaji.
Bendtner,
ambaye hajaichezea 'The Gunners' kwa takribani miaka miwili iliyopita kutokana
na kutolewa kwa mkopo Sunderland na baadaye Juventus, alionekana kama
angeondoka Kaskazini mwa London majira haya ya joto.
Wenger
amebaki na washambuliaji wawili tu, Olivier Giroud na Yaya Sanogo, baada ya
Lukas Podolski kuelezwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 10, kutokana na
kuwa majeruhi kufuatia kuumia kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya
Fenerbahce ambayo Jumanne walishinda 2-0 .
Ingawa
alitoa kipaumbele kwa kusajili mshambuliaji majira haya ya joto, Wenger sasa
analazimika kumrejesha Bendtner baada ya kushindwa kuwasajili Luis Suarez,
Wayne Rooney na Gonzalo Higuain.
"Nafasi
yake ya kuondoka kwa sasa ni ndogo sana, na kama atarejea na nikamuona yupo
fiti, nitamtumia," alisema Wenger akimzungumzia nyota huyo wa Kimataifa wa
Denmark.
"Hatutapaniki
kwa kununua, huo ndiyo uhakika. Unaweza kuniamini. Ninaweza kukupa simu yangu
na utaona kuwa nilikuwa na zaidi ya wachezaji 50 nilikuwa natarajia kuwasajili
mwisho wa siku.
"Ni
mwenye furaha kabisa kwa kile tunachokifanya na kwa namna tunavyofanya mambo
yetu. Siwezi kushiriki katika ukosoaji unaofanywa katika mchakato wangu wa
usajili kwa timu."
No comments:
Post a Comment