Bayern Munich imepata
majanga, baada ya mechi ya Ijumaa ya Uefa Super Cup dhidi ya Chelsea, kuibuka
mabingwa huku ikiwapoteza wachezaji wake nyota watatu kutokana na kuwa
majeruhi.
Viungo
Arjen Robben, Javi Martinez na Mario Gotze wote hawataweza kujifua na wenzao
wiki ijayo, huku Mjerumani Gotze akielezwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa wiki
tatu.
Mchezaji
wa Kimataifa wa Hispania, Martinez ambaye aliifungia Bayern bao la pili la
kusawazisha kwenye mechi hiyo, atayakosa mazoezi kwa muda wa siku tano zijazo
kutokana na maumivu ya goti.
Daktari
wa timu, Hans-Wilhelm Muller-Wohlfahrt pia aliagiza Robben, ambaye katika mechi
hiyo alitolewa dakika ya sita ya muda wa nyongeza kutokana na maumivu ya goti,
kupewa muda wa mapumziko.
@@@@@@@@@
Juan
Mata kuamkia Arsenal
London,
England
Juan Mata leo
itamlazimu kulazimisha kuomba kuondoka, ili kumwezesha kuamkia Arsenal kesho,
anaripoti Dave Kidd wa Gazeti la Sunday People.
Wiki
iliyopita, Sunday People Sport, lilieleza kutambua kuwa 'The Gunners' inataka
kumsajili nyota huyo raia wa Hispania, anayeichezea Chelsea na Jumanne Arsene
Wenger kuthibitisha hilo.
Lakini
Mata anakabiliwa na wakati mgumu kwa kutambua kuwa hataweza kupata nafasi ya
kuanza mara kwa mara katika Kikosi cha Chelsea chini ya Jose Mourinho, huku
akijua pia hataweza kuuzwa kabla ya dirisha la usajili la majira haya ya joto
kufungwa.
Mata,
25, ni kipenzi kikubwa cha mashabiki wa wakali hao wa Stamford Bridge, lakini
Mourinho ameweka bayana kuwa Oscar na Eden Hazard moja kwa moja watakuwa chaguo
lake la kwanza katika safu ya viungo watatu washambuliaji.
Mhispania
huyo aliwekwa benchi wakati 'The Blues'
ikiukosa ubingwa wa Super Cup dhidi ya Bayern Munich Ijumaa.
Katika
Kikosi cha Hispania kilichoitwa kujiandaa na mechi za kuwania kufuzu Kombe la
Dunia, Mata hakujumuishwa, lakini lengo lake ni kuona akishiriki fainali hizo
nchini Brazil majira ya joto yajayo.
Hivyo,
wakati huu ambao Arsenal imeonesha nia yake ya kumsajili kwa pauni milioni 30
(sh. bilioni 62.7 za Tanzania), Mata atalazimika kuomba kuondoka ili kuweza
kuamkia Emirates kesho kabla ya dirisha la usajili kufungwa leo saa sita usiku.
No comments:
Post a Comment