Joseph
amerejea kwenye timu hiyo baada ya kumaliza mkataba na Klabu ya Kongsvinger ya Norway,
hivyo leo atakuwa mmoja wa wachezaji ambaye atatambulishwa kwa mashabiki
kupitia mechi hiyo.
Wachezaji
wengine ni beki wa Kimataifa Mrundi, Gilbert Kaze na Mshambuliaji mwezake,
Amissi Tambwe waliotoka katika klabu ya Vital’O ya Burundi, ambao hawakuwemo
katika utambulisho mpya wa wachezaji wa timu hiyo kwenye tamasha lao la Simba Day.
Akizungumza
na BINGWA jana, Ofisa Habari wa Simba,
Ezekiel Kamwaga, alisema baada ya kucheza mechi mbili za Ligi Kuu Tanzania
Bara, wamerejea Dar es Salaam kujiandaa na mechi inayofuata dhidi ya Mtibwa
Sugar itakayochezwa Septemba 14, mwaka huu.
Kamwaga
alisema mechi hiyo itakuwa na faida kwao
kutokana na kujiandaa kuivaa Mtibwa, ikiwa ni baada ya kutoka sare ya
mabao 2-2 na Rhino Rangers na baadaye kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
JKT Oljoro.
Alisema
mechi hiyo itatoa nafasi kwa wapenzi na wanachama wa Simba, pamoja na mashabiki
wa soka kwa ujumla, kupata fursa ya kuwaona kwa mara ya kwanza wachezaji hao
ambao hawajawahi kuonekana wakicheza jijini Dar es Salaam.
Viingilio
vya mechi hiyo, vitakuwa ni Sh 20,000 kwa VIP A, Sh 10,000 kwa VIP B, Sh 8,000
kwa VIP C na Sh 5,000 kwa mzunguko.
Wakati
huo huo, alisema mechi hiyo itatumika na klabu kwa ajili ya mchezaji wake,
Kiggi Makassi, ambaye atawaaga kabla ya kwenda nchini India, Septemba 9, mwaka
huu, kwa ajili ya matibabu ya goti.
No comments:
Post a Comment