LONDON, England
KOCHA wa
Arsenal, Arsene Wenger, amesema Gunners wamepangwa kwenye kundi gumu na
kuongeza kuwa itakuwa ngumu kwa wao kuweza kufuzu hatua ya makundi, kutokana na
ubora wa timu zote nne.
Wenger,
aliweka wazi kuwa kufuzu katika hatua hiyo itakuwa kazi ngumu na kuna uwezekano
mkubwa wa kutolewa mapema.
Gunners
walitarajiwa kuanza na Olympique de Marseille na kusema kuwa itakuwa ngumu kwa
timu zilizopo kwenye kundi lao la F kuweza kunyakua pointi ugenini. Timu
nyingine za Kundi F ni Napoli na
Borussia Dortmund.
@@@@@@@@@@@@
Rooney hajui kama
atabaki Old Trafford
LONDON, England
PAMOJA na
mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney, kufikisha mabao 200 kwenye
klabu hiyo, lakini nyota huyo hajui hatima yake ndani ya Old Trafford.
Rooney
alifikisha mabao hayo 200, baada ya kupachika mabao mawili katika mchezo wa
Ligi ya Mabingwa ambao waliibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Akiwa
katika kiwango kizuri, Rooney aliisaidia United kwa kupachika mabao hayo mawili
na kutengeneza bao la nne, ambalo lilifungwa na Antonio Valencia, wakati kocha
mpya wa United, David Moyes, akipata ushindi wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa.
Lakini,
alipoulizwa na mtangazaji wa televisheni ya ITV, Gabriel Clarke, kama atabaki
Old Trafford, baada ya tetesi nyingi za kuwa ataondoka, Rooney alijibu kwa
ukali: “Sikiliza, ninaangalia masula yangu ya soka kama
ambavyo nimekuwa nikifanya misimu yote.
“Nimejinyenyekeza
ili niweze kufanya kazi kwa bidii na kujiweka fiti kwa ajili ya msimu huu.
Nimefurahishwa jinsi ambavyo nimerejea uwanjani na kutingisha nyavu.”
Lakini
baadaye, Rooney aliweka wazi katika mtandao wake wa Twitter kuwa amepanga
kubaki Old Trafford: “Ni matokeo mazuri leo usiku. Najivunia kuifungia United
mabao 200. Nina matumaini mengine mengi yatakuja.”
Mtangazaji
huyo, aliendelea kumbana Rooney ili aweke wazi kama ni kweli aliomba kuondoka
Manchester United majira ya joto, baada ya kocha wake wa zamani, Sir Alex
Ferguson, kusema kuwa mshambuliaji huyo anataka kuondoka na Chelsea kutuma ofa
mbili kwa ajili ya mchezaji huyo.
“Sikiliza,
tayari nimekwishakwambia,” alijibu Rooney, “Niko ‘bize’ na kutandaza soka kama
ambavyo nimekuwa nikifanya misimu yote.”
Utambi
ulichochewa zaidi, baada ya Moyes kutakiwa kueleza kama
Rooney ana furaha kubaki United na kuitumikia kwa muda mrefu.
“Sijui,”
alijibu Moyes. “Amekuwa akifanya vizuri katika mazoezi, akijituma kwa bidii,
anaonekana kuwa fiti na aliyejinyenyekeza. Nafikiri Robin van Persie na yeye
kwa pamoja ni wachezaji wazuri.”
Rooney
alipumzishwa baada ya dakika 86 na kushangiliwa sana na mashabiki wa Old
Trafford na Moyes, alikiri kuwa amefurahishwa na mchango wa mshambuliaji huyo
na kumpongeza kwa kufikisha mabao 200 ndani ya Old Trafford.”
No comments:
Post a Comment