LONDON, England
MSHAMBULIAJI
wa Manchester United, Robin van Persie, amemsifia mchezaji mwenzake, Wayne
Rooney, baada ya United kushinda mabao 4-2 katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya
Mabingwa, uliopigwa Jumanne.
Nyota
huyo wa Uholanzi, alipachika bao lake la sita katika msimu huu dhidi ya Bayer
Leverkusen, katika mechi hiyo ya kwanza hatua ya makundi, lakini Rooney,
alikuwa nyota wa mchezo kwa kutingisha nyavu mara mbili na kuweza kufikisha
mabao 200 katika klabu hiyo.
Kwa sasa
nyota huyo wa England,
Rooney, amekuwa mtu wa nne katika rekodi ya wachezaji wenye mabao mengi katika
historia ya klabu ya United, jambo ambalo limemfurahisha mchezaji huyo na Van
Persie amefurahia kucheza na mshambuliaji huyo.
“Wayne alicheza vizuri,”
aliiambia televisheni ya MUTV. “Napenda kucheza naye kwa kuwa anaweza kufanya
kila kitu, anaweza kurudi nyuma, anaweza kucheza pasi ndefu na fupi. Alicheza
vizuri sana.”
Pia
nyota huyo wa Uholanzi alimsifia mchezaji wao mpya, Marouane Fellaini, ambaye
alicheza vizuri kwa dakika 80.
“Naye
Marouane alicheza vizuri pia,” aliongeza Van Persie. “Alikuwa ngangari na
alinasa mipira mingi. Anacheza kwa kujiamini na kila wakati alikuwa akijaribu
kupeleka mipira mbele.”
@@@@@@@@@@
Coutinho kukosa mechi sita Liver
LIVERPOOL,
England
KIUNGO
wa Liverpool, Philippe Coutinho, atakuwa nje hadi mwishoni mwa Oktoba, baada ya
kuumia bega katika mchezo wa Ligi Kuu England
dhidi ya Swansea.
Nyota
huyo mwenye umri wa miaka 21, alitolewa nje katika mchezo uliomalizika kwa sare
ya mabao 2-2 kwenye uwanja wa Liberty,
baada ya kugongana na Ashley Williams.
Jopo la
madaktari wa Reds, wameamua kumfanyia upasuaji kwenye kiungo, ambapo itamfanya
nyota huyo wa Brazil
kukosa mechi sita.
Kocha
Brendan Rodgers, amefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England, bila
ya mshambuliaji wake, Luis Suarez, aliyefungiwa mechi 10, baada ya kumng’ata
beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, msimu uliopita.
Nyota
huyo wa Uruguay
anajiandaa kurejea dimbani katika mchezo wa Capital One Cup dhidi ya Manchester
United, utakaochezwa Jumatano ijayo.
Coutinho,
ametoa mchanganuo mkubwa kwenye kikosi cha Rodgers tangu alipowasili Januari
mwaka huu akitokea Inter Milan.
@@@@@@@@@@@@
Messi hajaomba kuongezwa mshahara
BARCELONA, Hispania
RAIS wa
Barcelona, Sandro Rosell, amesema kuwa mshambuliaji wake, Lionel Messi,
hajaomba kuongezwa mshahara, baada ya Real Madrid kumfanya Cristiano Ronaldo
mchezaji bora anayelipwa zaidi duniani.
Juzi
Jumapili, Ronaldo, alisaini mkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya dola
milioni 21 kwa msimu na kuwa mwanasoka anayelipwa zaidi na kuibua tetesi kuwa
huenda Messi akaomba kuongezewa mshahara.
Rosell
alisema mkataba mpya wa Ronaldo, hausumbui lolote mkataba wa nyota wao wa Argentina, katika klabu hiyo ya Camp Nou.
“Mkataba
mpya wa Ronaldo haujaathiri ule wa Messi na hajasema lolote kwetu,” alikaririwa
Rosell.
“Ana
furaha na yuko kwenye klabu bora duniani.”
Rais
huyo wa Barca, yuko katika kujadili mkataba mpya wa Andres Iniesta na mchezaji
huyo anatarajiwa kusaini mkataba huo hivi karibuni.
@@@@@@@@@@@@@
Ramos amrudisha
Iker Casillas benchi
MADRID, Hispania
MAMBO
yamekwenda vibaya kwa mlinda mlango wa Real Madrid, Iker Casillas.
Huenda
akapoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu yake ya Taifa ya Hispania na
klabu yake ya Real Madrid,
baada ya kurejea uwanjani kwa mara ya kwanza tangu akae benchi kwa siku 238,
lakini aliishia kucheza dakika ya 13, baada ya kuumia mbavu.
Madrid walicheza mechi yao
ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Galatasaray nchini Uturuki, lakini
alikaa langoni dakika chache, baada ya kugongana na beki wake, Sergio Ramos,
wakati walipokuwa wakiokoa mpira wa krosi.
No comments:
Post a Comment