Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 19, 2013

KILIO CHA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED CHASIKILIZWA!! KUTENGEWA SEHEMU MAALUM KWA AJILI YA KUIMBA NYIMBO NA KUHAMASISHA TIMU YAO KUANZIA DAKIKA YA KWANZA MPAKA MECHI IMALIZIKE


Manchester United watafanya majaribio Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya UCL dhidi ya Real Sociedad kwa kuweka eneo moja la Jukwaa kuwa sehemu maalum ya Washabiki ambao watakuwa wakiimba Nyimbo za kuhamasisha. In charge: Manchester United have mounted robust defence of manager David Moyes
Mpango huu ulitaka kujaribiwa Siku za nyuma lakini ukapingwa na Polisi kwa vile eneo la Jukwaa lilopangwa kuwaweka Waimbaji lilikuwa ni maalum kwa Washabiki wa Timu za Upinzani na ilibidi Mashabiki hao wahamishwe na kuwekwa kwenye Jukwaa jingine nyuma ya Maeneo ya Mabenchi ya Ufundi wa Timu kitu ambacho Polisi walikiona ni hatari.

Lakini safari hii Klabu imeunga mkono ombi la Mashabiki wao wa kuwa na Jukwaa la Waimbaji ili kuongeza sauti katika kuhamasisha Timu yao kwenye Mechi.
Inatarajiwa eneo hilo maalum la Jukwaa kwa ajili ya Waimbaji litakuwa na Washabiki 1,400 kwenye upande wa Kusini Mashariki hapo Oktoba 23 wakati wa Mechi na Real Sociedad.

Nae Kiungo wa Man United, Michael Carrick, ameunga mkono hatua hii kwa kutoa kwenye Akaunti yake ya Twitter posti: “Ni wazo zuri sana kuwa na eneo la Waimbaji. Kama ningekuwa naenda kama Shabiki hapo ndio ningetaka niwe….!!”

No comments:

Post a Comment