West
Albion ndio walioanza kufunga bao la kuongoza kipindi cha pili dakika
ya 54 Baada ya Morgan Amalfitano wa West Albion kukatiza na kuwapiga
chenga mabeki wa United na kuachia shuti kali.
Baada
ya dakika 3 kupita mchezaji matata wa United Wayne Rooney akaachia frii
kiki kwa shuti kali ambalo limeingia moja kwa moja nyavuni. Dakika ya
67 Manchester United wakafungwa bao la pili na Saido Berahino kwa shuti
kali. Mpira umemaliza dakika 90
huku kocha Moyes akiwa anajiuliza maswali mazito sana akiwa kwenye
uwanja wake Old Trafford. Kipigo hiki cha Kwa Manchester United
kinawaporomosha chini zaidi huku West Bromwich wakipanda juu
Marouane Fellaini na Robin van Persie wa Manchester United wote wameanzia benchi mechi hii
Shinji Kagawa wa Manchester United akipambana na Scott Sinclair wa West Bromwich Albion
Javier "Chicharito" Hernandez wa Manchester United akipambana na Gareth McAuley kulia
Marouane Fellaini hoi baada ya Man United kufungwa bao la pili akiwa bado yupo benchi
Phil Jones wa Manchester United kwenye kasi na mpira akikabwa na Victor Anichebe wa West Bromwich
Rio Ferdinand akimkaba vilivyo mchezaji mdogo wa miaka 20 Saido Berahino wa West Bromwich
Rooney kushoto nae akikabwa na Saido Berahino

Bao la Saido Berahino, limewapa West Brom ushindi wao wa kwanza dhidi ya Manchester United Uwanjani Old Trafford tangu Mwaka 1978 kwa kushinda Bao 2-1.
Bao zote zilifungwa Kipindi cha Pili na WBA walitangulia kufunga kupitia Morgan Amalfitano na Wayne Rooney kusawazisha Dakika 3 baadae.
Marouane Fellaini aliweza kuisawazishia Man United lakini Bao hilo lilikatawaliwa kwa Ofsaidi na kuifanya Man United iwe imeanza vibaya Ligi kupita wakati wowote tangu Msimu wa 1989/90.













David de Gea kipa wa United kilio baada ya mtanange!!!

No comments:
Post a Comment