Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, September 17, 2013

LIVERPOOL ILIVYOTOKA SARE NA SWANSEA CITY MABAO 2 -2 LIVERPOOL YARUDI KILELENI

Ligi kuu England Jumatatu jana kulikuwa na mtanange mmoja wa pekee kati ya Swansea na Majogoo Liverpool wakiwa ugenini. Swansea City wakiwa kwao kwenye uwanja wa Liberty ndiyo waliotangulia kufunga bao la mapema dakika ya 2 kupitia mchezaji wao Shelvey aliyekatiza kwenye ngome ya Majogoo hao Liverpool na kufanya shambulizi la maana na kumfunga kipa wa Liverpool Mignolet. Muda mfupi baadaye mchezaji Danniel Sturridge akasawazisha bao hilo dakika ya 4 na kuwaziba mdomo mashabiki wa Swansea City, Huku Moses akimalizia bao la pili dakika ya 36. Kipindi cha kwanza kilimalizika Liverpool wakiongoza kwa bao 2-1 dhidi ya Swansea. Kipindi cha pili Pamoja na Liverpool kuja na nguvu zaidi ya Swansea kwa kufanya mashambulizi dakika ya 64 mchezaji hatari Michu akasawazisha bao na kufanya 2-2 na mtanange kuwa mgumu zaidi kwa Liverpool. Matokeo haya yanawarudisha tena Liverpool juu kileleni mwa ligi wakiwa na Alama 10 wakifuatiwa na Arsenal. Wao Swansea wapanda juu nafasi ya 13 na alama zao 4.Shelvey akiachia shuti kali ambalo limempita kipa kwa juu baada ya mabeki wa Liverpol kufanya makosa ya ukabaji.Jonjo Shelvey baada ya kuumiza kwa kutupia bao nyavuni!
Wachezaji wote wa Swansea wakipongezana na kumpongeza Shelvey aliyefunga bao la dakika za mapemaJonjo Shelvey akifurahia kwa kuwapa mkono mashabiki wa Swansea kwenye uwanja wao wa nyumbani Liberty Furaha zilitanda kwa Timu ya Swansea City Mnanionaee!!!Brendan Rodgers hoi!!!Daniel Sturridge....Sturridge akiachia shuti kali na kufanikiwa kumfunga kipa wa Swansea City Vorm Kazi kwenu!! kuibeba timu ni muhimu kwangu!Sturridge akiwazima mashabiki wa Swansea City
Moses akiutazama mpira unaoelekea nyavuni.!!Victor Moses akitupia bao la 2 Moses akishangilia kwa aina yake huku akimsogelea kocha wake Brendan Rodgers Mtaisoma namba!!Jonjo hoi!!Jonjo kipindi cha pili aliwakaba kisawasawa LiverpoolSteven Gerrard akichuana na mchezaji wa SwanseaCoutinho akitupwa chini Miguel Michu kwenye patashika hapa wakati anasawazisha bao la 2Michu akipeta na kushangilia baada ya kusawazisha bao na kufanya 2-2 dakika ya 64 kipindi cha pili.Shelvey akifurahia baada ya Michu kusawazisha bao la pili!!Steven Gerrard .....Mh!!!Philippe Coutinho akiokoa hapa!!
VIKOSI:
Swansea: Vorm, Rangel, Flores, Williams, Davies, Britton, Shelvey, Michu, Dyer (De Guzman 46), Routledge, Bony (Pozuelo 66).
Subs: Tremmel, Amat, Tiendalli, Canas, Vazquez.
Booked: Williams, Shelvey.
Goal: Shelvey 2, Michu 64.
Liverpool: Mignolet, Wisdom (Toure 69), Skrtel, Sakho, Enrique, Lucas, Gerrard, Henderson, Coutinho (Aspas 54), Moses (Sterling 81), Sturridge.
Subs: Jones, Alberto, Ibe, Kelly.
Booked: Lucas, Henderson, Wisdom.
Goal: Sturridge 4, Moses 36.

RATIBA -MATOKEO
Jumatatu 16 Septemba
Swansea City 2 v Liverpool 2

RATIBA: LIGI KUU ENGLAND WIKI IJAYO!
Jumamosi 21 Septemba
14:45 Norwich City v Aston Villa
17:00 Liverpool v Southampton
17:00 Newcastle United v Hull City
17:00 West Bromwich Albion v Sunderland
17:00 West Ham United v Everton
19:30 Chelsea v Fulham
Jumapili 22 Septemba
15:30 Arsenal v Stoke City
15:30 Crystal Palace v Swansea City
18:00 Cardiff City v Tottenham Hotspur
18:00 Manchester City v Manchester United

No comments:

Post a Comment