KLABU
ya AC Milan imetangaza katika mtandao wake kuwa kiungo wake nyota Kaka
atakuwa nje ya uwanja kwa muda baada kupata matatizo ya msuli katika
mchezo dhidi ya Torino mwishoni mwa wiki iliyopita. Kiungo huyo
alilazimika kutoka nje ya uwanja baada ya kucheza kwa dakika 70 katika
mechi yake ya kwanza toka arejee katika klabu hiyo na kufanyiwa vipimo
zaidi na kuthibitisha ukubwa wa tatizo lake. Madaktari
wa Milan wataendelea kumfanyia vipimo zaidi nyota huyo kwa siku 10
kabla ya kutaja tarehe rasmi atakayoweza kurejea tena uwanjani. Mapema
Kaka amesema alizungumza na viongozi wa Milan na kuweka wazi kuwa
hatakuwa akichukua mshahara wake kama atakuwa hachezi kutokana na kuwa
majeruhi atakachohitaji yeye ni klabu kumsaidia katika kipindi hicho ili
aweze kurejea katika hali yake ya kawaida. Kwasasa
Milan inakabiliwa na wachezaji wengi majeruhi akiwemo Giampaolo
Pazzini, Daniele Bonera, M’Baye Niang, Riccardo Montolivo, Mattia De
Sciglio, Ignazio Abate na Stephan El Shaarawy.
No comments:
Post a Comment