
Bao la pekee la dakika ya 46 la Chicharito limetosha kuwapa ushindi United walipocheza na Liverpool usiku huu kwenye ligi ya Mtoano Capital One Cup, Kona iliyopigwa mapema kipindi cha pili na Wayne Rooney na hatimaye hatimaye Chicharito kuunganisha hadi kona hiyo moja kwa moja hadi nyavuni. Huku macho yote yakimwangalia Suarez Old Trafford ambaye leo ndiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza tangu apewe kifungo cha mechi kumi, licha ya kucheza vizuri hakuweza kufunga bao. Kipindi cha kwanza licha ya United kucheza kwa kasi hawakuweza kufungana na Liverpool hatimaye kipindi hicho kiliisha ya bila kufungana na Mahasimu hao Liverpool. Ushindi huu pia unaondoa maswali mengi na utata uliokuwepo kwa United kucheza kwa kusuasua karibu mitanange mitatu iliyopita.













Suarez akifanya mazoezi mapema kabla ya mtanange kuanza.
RATIBA/MATOKEO
Jumatano Septemba 25
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Birmingham 3 v 0 Swansea
Manchester United 1 v 0 Liverpool
Newcastle 2 v 0 Leeds
Tranmere 0 v 2 Stoke
[Saa 4 Usiku]
West Brom 1 v 1 Arsenal(penati 3-4)
No comments:
Post a Comment