Baada
ya kutoshana nguvu kwa bao 1-1 katika dakika 90 ziliongezwa dakika 30
tena na ambazo pia wametoka sare ya bila kufungana. Bao la Arsenal
limefungwa dakika ya 61 na Thomas Eisfeld huku West Brom wakisawazisha bao hilo baada ya dakika 10 kupitia mchezaji
Saido Berahino katika dakika ya 71. Matuta
ndiyo yalifata Arsenal wakikosa mkwaju wa pili na wao West Brom
wakikosa mkwaju wa nne baada ya mchezaji kupaisha nje ya lango pamoja na
mkwaju wa tano. Arsenal wamesonga mbele baada ya kupata mkwaju wa nne
na watano na hatimaye kusonga mbele kwenye hatua ya raundi ya nne ya
mtoano. kwenye mitanange mingine iliyochezwa leo Manchester United
wameifunga bao 1-0 Liverpool, Birmingham wameifunga bao 3 kwa 0 Swansea, Newcastle wameifunga bao 2-0 Leeds na Stoke City wameifunga bao 2-0 Tranmere.
Nicklas Bendtnerakisalimiana na wenzake kabla ya mtanange
Kipindi cha kwanza kilimalizika 0-0
Mwangalie Bendtner akicheza na Arsenal kwa mara nyingine leo baada ya siku 767 kupita!!
Majanga!!
RATIBA/MATOKEO
Jumatano Septemba 25
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Birmingham 3 v 0 Swansea
Manchester United 1 v 0 Liverpool
Newcastle 2 v 0 Leeds
Tranmere 0 v 2 Stoke
[Saa 4 Usiku]
West Brom 1 v 1 Arsenal(penati 3-4)
No comments:
Post a Comment