MKURUGENZI wa Fedha na Utawala wa klabu ya Yanga, Denis
Oundo jana alizindua tawi la Yanga, la Mfenesini lililopo Mbagala, jijini Dar
es Salaam.
Denis Oundo ambaye alikuwa amefuatana na Ofisa Habari wa
Yanga, Baraka Kiziguto na meneja wa timu ya Yanga, Hafidh Salehe walipokelewa
kwa maandamano toka Mbagala hadi Kiburugwa huku wakiwa wamebeba kombe ambalo la
Ubingwa la Yanga la 2012/13.
Akizungumza wakati akizindua tawi hilo, Oundo alisema
anawapongeza wanachama hao kwa kuweza kuwa na wazo la kuwa na tawi kwani
litakuwa kiungo kati ya wanachama na Makao makuu.
“Nawapongeza kwa kuanzisha tawi kwani itawasaidia ninyi
kupata taarifa mbalimbali kupitia uongozi wenu hivyo wengine waige mfano wenu”,
alisema Oundo.
Naye Makamu Mwenyekiti wa tawi hilo, Alphonce Rwena alisema
wao wameanzisha tawi hilo ili lisaidie kuinua maendeleo ya klabu yao na kujenga
umoja kwa wanachama.
“Sisi lengo letu kuanzisha tawi hili ni kujenga ushirikiano
kati ya wanachama wa Yanga waliopo Kiburugwa na wanachama wengine na lengo
lingine ni kuanzisha academi ambayo itakuwa inatoa wachezaji ambao wanaweza
kusaidia Yanga”, alisema Rwena.
No comments:
Post a Comment