MWENDESHA Baiskeli kutoka Mkoa wa Mwanza,Masunga Duba ameibuka bingwa katika mashindano ya mbio za baiskeli Kanda ya Ziwa Wanaume zinazojulikana kwa Safari Bike Race 2013.
Masunga aliibuka bingwa katika mbio hizo zenye umbali wa kilometa 210 kutoka Mkoani Shinyanga na kurudi kwa muda wa saa 6:01,zilizojumuisha mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Kigoma,Tabora,Shinyanga,Geita,Simiyu,Kagera na Mara na hivyo kujinyakulia fedha taslimu shilingi 1,00,0000/=.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni Charles Clement kutoka Shinyanga ambeye alitumia muda wa saa 6:02 na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 800,000/=,mshindi wa tatu ni Bernadi Mwigulu kutoka Shinyanga alitumia muda wa saa 6:03 na kuzawadiwa shilingi 600,000/=,mshindi wa nne ni Gilisi Juma kutoka Shinyanga alitumia saa 6:04 na kuzawadiwa shilingi 500,000/=,mshindi wa tano Mhindi Ngwagi kutoka Simiyu alitumia saa 6:05 na kuzawadiwa shilingi 300,000/= na washindi wa sita mpaka kumi walipewa kifuta jasho cha shilingi 100,000/=kila mmoja ambao ni Mungu Ataleta alitumia saa 6:06,Paul John alitumia saa 6:07,Ngosele Luhanga alitumia saa 6:08,Bingwa mtetezi Seni Konda alitumua saa 6:09 na Hamisi Clementi ambaye alitumia saa 6;10.
Upande wa Waanawake ambao walikimbia mbio za kilometa 130 kutoka Shinyanga mpaka Nzega Ngogo,Martha Anthon kutoka Mwanza aliibuka bingwa ambaye alitumia muda wa saa 4:37 na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 700,000/=,mshindi wa pili ni Nyanzobe Masanja kutoka Shinyanga alitumia muda wa saa 4:49 na kuzawadiwa shilingi 500,000/=,wa tatu niHalima Juma kutoka Mwanza alitumia saa5:01 na kuzawadiwa shilingi 300,000/=,wa nne ni Bertha Bernard kutoka Shinyanga alitumia saa 5:04 na kuzawadiwa shilingi 200,000/=,wa tano ni Salma Kashinje alitumia saa 5:10 na kuzawadiwa shilingi 150,000/=,washindiwa wa nafasi ya sita mpaka 10 walizawadiwa kifuta jasho cha shilingi 100,000/= kila mmoja ambao ni Flora Seleli kutoka Shinyanga alitumia saa 5:12,Pili Mpanduji kutoka Shinyanga alitumia saa 5:14,Maaria Matias kutoka Shinyanga alitumia saa 5:25, Laurencia Luzuba kutoka Mwanza alitumia saa 5:30 naMagreth Elias kutoka Shinyanga ambaye alitumia saa 6:09.
Mashindano hayo pia yalijumuisha walemavu wanaume na wanawake ambao walijinyakulia zawadi mbalimbali kutoka kwa wadhamini TBL kupitia bia ya Safari Lager.
Akitoa hutuba Mgenirasmi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Kaimu Kaimu katibu tawala Rasilimali na Watu wa Shinyanga, Projestas Lubanzibwa aliishukuru Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia Bia ya Safari Lager kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo kwani kila mwaka yamekuwa yakiboreshwa na kuyafanya yawe na mvuto kwa washiriki na wakazi wa kanda ya Ziwa.
Alisema Lubanzibwa,zawadi zilizotolewa tayari ni mtaji kwa Yule aliyepata wa kuanzisha biashara yoyote na si hilo tu mmeongeza mapenzi kwa fammilia ziliofanikiwa kupata zawadi hizo katika kipindi cha sikukuu ya nane nae na Idd kwa namna moja ama nyingine,lakini pia Serikari inatambua mashindano hayo kwani Umati unafika Uwanjani kushuhudia ni dhahili mashindano wanayapenda.
Lubanziba mwisho akatoa wito kwa TBL kuendelea kudhamini mashindano hayo kwani yanaleta ungugu kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kwani michezo ni furaha,michezo ni afya na michezo ni ajira. Nae Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kanda ya Ziwa aliwashukuru wakazi wa Kanda ya Ziwa kwa mshikamano wanaounyesha katika kushiriki na kushuhudia mashindano hayo ambayo yanafana mwaka hadi mwaka na kuwaomba wakazi wa Kanda ya Ziwa kutumia Bia ya Safari Lager ili indelee kudhamini mashindano hayo na kuboresha zawadi zaidi.
No comments:
Post a Comment