Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, August 1, 2013

WAKALI SABA WANAOWEZA KUZIBA PENGO LA SUAREZ

LONDON, England

KLABU ya Liverpool bado imeweka ngumu kumwachia nyota wake, Luis Suarez ang’oke kwenye klabu hiyo.

Wakati Liverpool ikiweka ngumu, nyota wengine Ulaya mambo yameshawanyookea, baada ya kusaini mikataba mipya ama kuhamia kwenye klabu nyingine.

Miongoni mwa wachezaji ambao mambo yao yameshakuwa safi ni pamoja na mfungaji bora wa ligi ya  Bundesliga msimu uliopita, Stefan Kiessling, ambaye amesaini mkataba mpya na klabu yake ya Bayer Leverkusen, huku Robert Lewandowski akijiandaa kujiunga na Bayern Munich msimu ujao, wakati  Stevan Jovetic, Gonzalo Higuain, David Villa na Alvaro Negredo wote wakiwa wameshakamilisha usajili.

Mbali na wachezaji hao, timu ya Juventus yenyewe imeshamnasa Fernando Llorente na nyota wa  Manchester City, Carlos Tevez, ambao ni kati ya nyota wazuri  Ulaya.

Hata hivyo, endapo kocha Brendan Rodgers ataamua  kumuachia aondoke kwenye klabu hiyo ya Anfield, swali lililopo ni kwamba ni nyota gani atakuwa mbadala kwa Suarez?

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya soka, wanaangazia wachezaji saba ambao wanaweza kuziba pengo la Suarez endapo ataondoka.


Jackson Martinez
Jackson Martinez
Mcolombia huyo mwenye misuli,  Martinez msimu uliopita alifunga mabao  26 katika mechi  30 alizoichezea FC Porto na mabao hayo ndiyo yalimfanya kuwa mchezaji anayewindwa kwa udi na uvumba katika soko la usajili.

Inaelezwa kuwa endapo Suarez ataondoka, inambidi Rodgers  kwa haraka kukimbilia kumsajili nyota huyo hususan  baada ya Rais wa Napoli,  Aurelio De Laurentiis naye kuthibitisha nia ya kumsajili.

Inaelezwa pia uwezo wa kutoa pasi na nguvu alizonazo unaweza kuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha Liverpool.


Luis Muriel
Luis Muriel
Akiwa tayari ameshaonesha uwezo kama mchezaji raia mwenzake, Falcao  na nyota wa  Brazil,  Ronaldo, Muriel anatajwa kuwa hazina kwenye mechi.
Mwaka jana katika msimu wake wa kwanza akiwa na timu ya Udinese aliweza kupachika mabao 11 na mara kadhaa amekuwa akitolewa macho na klabu kubwa.

Inaelezwa kuwa akiwa na umri wa miaka 22, huenda akawa hazina kwa timu hiyo endapo kocha wake ataamua kumnunua.


Roberto Soldado
Roberto Soldado
SOLDADO  ameshadhihirisha uwezo wake wa kuweka rekodi, baada ya kufunga mabao  81 katika mechi  141 alizoichezea Valencia.
Tayari kocha wa Tottenham, Andre Villas-Boas ameshakiri kummezea mate mshambuliaji huyo, lakini klabu hiyo ya Hispania imeshaweka ngumu hadi dau lake la pauni milioni 26 litakapokamilika kabla ya kumuachia aondoke.

Inaelezwa kuwa kuwa hata kama hataweza kuwa mbadala halisi wa  Suarez, lakini kwa uwezo wa Mhispania huyo aliouonesha hivi karibuni unakuwa na uhakika wa hela yako kurudi.


Oscar Cardozo
Oscar Cardozo
Kinara huyo raia wa  Paraguay aliwateka mashabiki wa Benfica  baada ya kupachika mabao misimu yote sita mfululizo aliyoichezea timu hiyo ya  Estadio da Luz.
Hata mwishoni mwa msimu uliopita alijikuta kwenye wakati mgumu, baada ya kukwaruzana na kocha wake, Jorge Jesus.

Kutokana na uwezo wake, Fenerbahce inatamani kumsajili Cardozo ambaye pia anawindwa na timu ya  Cardiff City, lakini ikakataa kutoa ofa zaidi ya milioni 13 kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30.

Inaelezwa kuwa mwajiri wake huyo Mreno anasemekana anataka kitita cha pauni milioni 15 ili imwachie nyota huyo ambaye licha ya kutokuwa na uwezo mkubwa wa kutoa pasi, lakini anaweza kufanya makubwa kwenye kikosi hicho cha  Anfield.

Leandro Damiao
Leandro Damiao
Mshambuliaji huyo wa timu ya Inter Milan, Mbrazili mwenye umri wa miaka 24, ameshindwa kuonesha cheche zake kwenye kikosi cha timu ya taifa kama alivyo shujaa  Fred kutokana na kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara.

Akiwa anawindwa kwa  muda mrefu Spurs, Damiao wakati mwingine amekuwa akiwindwa na vigogo kadhaa  vya Ligi Kuu, lakini klabu yake imekuwa ikiweka ngumu kumuuza kwa bei chee.

Inaelezwa kuwa licha ya kukumbwa na majeraha, lakini endapo atatumika vilivyo anaweza kuwa tishio kwa mabeki.

Pablo Osvaldo
Pablo Osvaldo
Mshambuliaji huyo, Osvaldo amekuwa akihusishwa kuhamia katika timu za Fulham na  Valencia, lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa.

Akiwa na umri wa miaka  27, msimu uliopita aliifungia timu yake ya AS Roma mabao 16  kwenye michuano ya Ligi ya Serie A na ameshaichezea mara nane timu ya Taifa ya Italia.


Inaelezwa kuwa endapo Rodgers atamnyakua mzaliwa huyo wa Argentina, anaweza kuwa msaada mkubwa kwake kama ilivyo kwa Suarez.


Fred
Fred
Akiwa na umri wa miaka  29, anaweza kuwekwa kando kwa wachezaji chipukizi wa Rodgers.
Lakini hata hivyo inaelezwa mshambuliaji huyo bado ana uwezo wa kufanya makubwa.


No comments:

Post a Comment