KATIBU Mkuu wa zamani wa Chama cha soka Tanzania (FAT) hivi sasa Shirikisho
la soka Tanzania (TFF), Michael Wambura
ameshindwa kujitosa katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi yoyote ndani ya taasisi
hiyo baada ya kushindwa kutokea kwenye
zoezi la uchukuaji na urejesaji wa fomu lililofungwa jana jioni.
Awali kwenye kinyan’ganyiro cha kwanza cha uchaguzi huo, ambao mchakato
wake ulivurugika, Wambura alijitosa kugombea nafasi ya Makamu wa Urais nafasi
ambayo ilikuwa ikiwaniwa na Nassib Ramadhani na Wallace Karia.
Pia katika uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board), unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 18 mwaka huu, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji naye
ameshindwa kujitosa katika kinyan’ganyiro cha uchaguzi huo, kama alivyofanya
awali katika mchakato wa kwanza.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura alilieleza DIMBA kwamba jumla ya wadau wa soka 58 wamejitokeza
kuomba ridhaa ya kuwania nafasi mbalimali kwenye uchaguzi huo.
Baadhi ya
walioomba ridhaa hiyo Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na
Richard Rukambura ambao wameomba kuwania nafasi ya Urais huku nafasi ya Makamu
wa Rais wamejitokeza Imani Madega, Nasib Ramadhani na Wallace Karia.
Baadhi ya wagombea
kwenye nafasi za ujumbe ni pamoja na Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Samwel
Nyalla, Ally Mtumwa,
Ahmed Mgoyi, Ayoub
Nyenzi, Cyprian Kuyava, Eliud Mvela, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, Davis Mosha, Juma
Pinto, Muhsin Balhabou, Omar Abdulkadir, Shaffih Dauda na Wilfred Kidao.
Kwa upande wa TPL
Board waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni Hamad Yahya (Mwenyekiti) na Said
Muhamad (Makamu Mwenyekiti).Walioomba nafasi za ujumbe ni Kazimoto Muzo,
Michael Kaijage, Omari Mwindadi, Salum Rupia na Silas Magunguma.
No comments:
Post a Comment