Tuesday, August 20, 2013
BENNI McCARTHY ANAMKUBALI MOURINHO
KLABU ya
Porto ya Ureno ilipata mafanikio makubwa ikiwa chini ya Kocha Mkuu wa sasa wa
Chelsea, Jose Mourihno huku baadhi ya wachezaji waliotoa mchango kwenye timu
hiyo akiwa ni McCarthy ambaye alishaitumikia Timu ya Taifa ya Afrika Kusini
maarufu kama Bafana Bafana.
Katika
mahojiano na gazeti moja la The Guardian la Afrika Kusini, McCarthy anasema
kuwa Jose Mourihno ni kocha mzuri, kwani katika kipindi cha misimu miwili
kuanzia 2002 hadi 2004 aliyokaa na Porto aliiwezesha kupata mafanikio ikiwa ni
pamoja na kuiwezesha kutwaa taji la UEFA na taji la Mabara.
“Kucheza
soka kumenifanya niwe katika hali nzuri na kuweza kuinua maisha mazuri pamoja
na familia yangu, hivyo kwa mafanikio hayo mchezo huo nauheshimu na kuupenda.
“Nimefurahia
mno maisha yangu ya soka ambayo yalitoa kutoka katika timu za mtaani na
hatimaye baadaye kuiwezesha klabu yangu ya Porto ambayo nilikuwa naichezea
kutwaa taji la UEFA na kuichezea timu yangu ya Taifa ya Afrika Kusini katika
michuano ya Kombe la Dunia, hivyo hayo ni mafanikio makubwa,” anasema McCarthy.
McCarthy
akitokea katika mazingira ya kimasikini katika timu za mchangani hadi kuchezea
katika ligi kuu kama za Hispania, Ureno, England na kutwaa Mataji akiwa na Ajax
ya Uholanzi na Porto ya Ureno.
Pamoja na
kuichezea klabu ya Porto ya Ureno kwa mafanikio makubwa, pia timu ya Taifa ya
Afrika Kusini wanafahamu mchango wake, baada ya kudumu nayo kwa muda wa miaka
miaka 16 kuanzia 1997 hadi 2012, akicheza mechi 79 na kufunga mabao 32.
McCarty
ambaye alistaafu soka akiwa na umri wa miaka 35 ana mambo mengi ya kujivunia
lakini akiwa na ameshapachika mabao 161 baada ya kushuka dimbani mara 387
zikiwemo mechi za timu ya taifa.
Katika
michuano ya fainali za Mataifa huru Afrika ya mwaka 1998 iliyofanyika nchini
Burkina Faso, McCarthy pamoja na mshambuliaji wa Misri, Hassan Hassan waliibuka
vinara kwa upachikaji wa mabao na McCarthy kutangazwa kuwa mchezaji bora wa
michuano hiyo.
Katika
fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1998 zilizofanyika nchini Ufaransa Bafana
Bafana mchezo wa kwanza ilifungwa Ufaransa ambao walikuwa Mabingwa wa taji hilo
mabao 3-0, mchezo wa pili dhidi ya Denmark katika dakika ya 13 walikuwa
wamefungwa bao moja, lakini katika dakika ya 52 McCarthy akisawazisha kuipa
matumaini ya kusonga mbele.
Lakini hata
hivyo katika mchezo wa tatu matumaini hayo yaliyeyuka baada kutoka sare na
Saudia Arabia na hivyo kutolewa baada ya kushika nafasi ya tatu.
McCarthy
akiwa na Bafana Bafana katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2002
zilizofanyika Korea na Japan, historia ya kutofanya vizuri ilijirudia, kwani
katika mchezo wa kwanza ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Paraguay, ilishinda
mechi ya pili bao 1-0 dhidi ya Slovenian, lakini ilijikuta ikiaga michuano hiyo
na kuwa mshindi wa tatu baada ya kufungwa na Hispania mabao 3-2.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment