Stephane Mbia,
amejiunga na klabu ya Sevilla kwa mkopo. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka
Cameroon, mwenye umri wa miaka 27, sasa ataichezea klabu hiyo ya Hispania msimu
huu wote. Mbia alijiunga na QPR, kutoka klabu ya Marseille mwaka uliopita, kwa
mkataba wa miaka miwili, naye Joey Barton akajiunga na Marseille msimu huo kwa
mkopo.
Aliicheza QPR mechi 32,
wakati klabu hiyo iliposhushwa daraja msimu uliopita. Mbia ni mchezaji wa Saba
kuihama klabu hiyo kwa mkopo au kwa mkataba wa kudumu tangu waliposhushwa
daraja. Katika miezi ya hivi karibuni, klabu hiyo imepoteza wachezaji wake
Christopher Samba, Djibril Cisse, Jose Bosingwa, Loic Remy, Esteban Granero na
Park Ji-sung. Mchezaji huyo kutoka Cameroon, alipigwa faini na QPR mwezi Mei
mwaka uliopita, wakati alipotuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter
akiashiria kuwa anataka kurejea Hispania na kuichezea klabu yake ya
zamani
No comments:
Post a Comment