REFA Jonas
Eriksson kutoka Sweden ametangazwa na UEFA kuwa ndiye Refa wa pambano la
UEFA Super Cup kati ya Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich na Washindi wa
EUROPA LIGI Chelsea litakalochezwa huko Stadion Eden Mjini Prague Nchini Czech
Republic hapo Ijumaa Agosti 30.
Eriksson, Miaka 39,
amekuwa Refa wa Kimataifa tangu Mwaka 2002 na ameshachezesha Mechi 75 za
UEFA.
Msimu uliopita,
Eriksson alichezesha Mechi 6 za UEFA CHAMPIONZ LIGI ikiwemo Robo Fainali kati ya
Málaga CF na Borussia Dortmund na pia kuchezesha Mechi 3 za EUROPA LIGI ikiwemo
Mechi ya pili ya Nusu Fainali kati ya Chelsea na FC Basel.
Kwenye Mechi hiyo
ya UEFA Super Cup, Eriksson atasaidiwa na wenzake kutoka Sweden Mathias
Klasenius na Daniel Wärnmark huku Stefan Wittberg akiwa Refa wa Akiba na
Wasaidizi wa Nyongeza ni Stefan Johannesson na Markus
Strömbergsson.
UEFA
SUPER CUP-WASHINDI WALIOPITA!
2012
Atlético
2011
Barcelona
2010
Atlético
2009
Barcelona
2008
Zenit
2007
Milan
2006
Sevilla
2005
Liverpool
2004
Valencia
2003
Milan
2002 Real
Madrid
2001
Liverpool
2000
Galatasaray
1999
Lazio
1998
Chelsea
1997
Barcelona
1996
Juventus
1995
Ajax
1994
Milan
1993
Parma
1992
Barcelona
1991 Manchester
United
1990
Milan
1989
Milan
1988
Mechelen
1987
Porto
1986
Steaua
1984
Juventus
1983
Aberdeen
1982 Aston
Villa
1980
Valencia
1979 Nottm
Forest
1978
Anderlecht
1977
Liverpool
1976
Anderlecht
1975 Dynamo
Kyiv
1973
Ajax
No comments:
Post a Comment