Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, August 16, 2013

MZEE WENGER AWATOA WASIWASI WANA GUNNERS KUWA WAPYA WATAKUJA!

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza Klabu yake itachacharika kwenye Soko la Uhamisho wa Wachezaji hadi mwisho wake hapo Septemba 2 litakapofungwa. 

Licha ya Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, kuahidi kumwaga Mamilioni Sokoni kununua Wachezaji wakubwa na wa bei mbaya, hadi sasa Arsenal imefanikiwa kumsaini mmoja tu ambae ni Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana ya France U-21, Yaya Sanogo, kutoka Auxerre kwa Uhamisho wa bure bila ya malipo.
Hata hivyo, hali hiyo haimkeri Arsene Wenger ambae ametoa mfano wa Chelsea na Manchester United ambao wako kwenye hali kama Arsenal: “Bado tunahangaika. Tupo kwenye hali kama ya Man United na Chelsea ambapo kila Mtu anategemea Wachezaji wapya watasainiwa lakini hakuna lililofanyika. Bado zipo Siku 18 zimebaki na hizo ni nyingi mno kwenye Soko la Uhamisho na tutashughulika hadi mwisho.” 

Lakini Wenger hakutaka kujifunga moja kwa moja kwa ahadi pale alipotamka: “Siwezi kuthibitisha Wachezaji wangapi watakuja lakini tutashughulika hadi mwisho na huo ni uhakika.”
Wakati huo huo, Wenger alitoboa kilichomfanya amuuze kwa Pauni Milioni 8 Fowadi wa Ivory Coast Gervinho kwenda AS Roma na kudokeza ni sababu ya kuzomewa kwake na Mashabiki wa Arsenal hasa alipokuwa akicheza Uwanja wa Emirates. 

Wenger amefafanua: “Nilifanya uamuzi ule kwa sababu alikuwa akicheza bila kujiamini hasa Uwanja wa Emirates. Ni Mchezaji mbunifu sana, mpiga chenga kiasilia na kwa hilo unahitaji kujiamini ili ucheze vizuri zaidi. Katika Miezi sita nilihisi ilikuwa ngumu kwake kuonyesha kipaji chake kwa njia ya kujiamini.” Michu pia alikuwa ni chaguo la Wenger msimu huuWakati huo huo Suarez anaonekana kubaki Liverpool akiwa ni Chaguo namba moja pia

ARSENAL'S CURRENT FIRST TEAM SQUAD

Goalkeepers: Szczesny, Fabianski.
Defenders: Mertesacker, Koscielny, Jenkinson, Gibbs, Vermaelen (inj), Monreal (inj), Sagna (inj).
Midfielders: Rosicky, Oxlade-Chamberlain, Wilshere, Ramsey (precaution), Cazorla (travelled from Ecuador), Arteta (inj), Diaby (inj), Frimpong*, Miyaichi (inj).
Forwards: Podolski, Giroud, Walcott, Sanogo (inj), Park*, Bendtner*.

THE GUNNERS' GREAT SUMMER EXODUS ...

PLAYERS OUT: Andrey Arshavin (released), Denilson (Sao Paulo, free), Sebastien Squillaci (released), Martin Angha (Nuremberg, undisclosed), Craig Eastmond (Colchester, free), Conor Henderson (released), Jernade Meade (Swansea, free), Sanchez Watt (Colchester, free), Johan Djourou (Hamburg, loan), Vito Mannone (Sunderland £2m), Andre Santos (Flamengo, free), Francis Coquelin (Freiburg, loan), Joel Campbell (Olympiacos, loan), Chuks Aneke (Crewe, loan), Marouane Chamakh (Crystal Palace, free), Ignasi Miquel (Leicester, season-long loan), Gervinho (Roma, £8m).
PLAYER IN: Yaya Sanogo (Auxerre, free).

No comments:

Post a Comment